Showing posts with label Adam Lallana. Show all posts
Showing posts with label Adam Lallana. Show all posts

Monday, 15 August 2016

EPL: LIVERPOOL YAIBUKA MSHINDI DHIDI YA ARSENAL KATIKA GAME KALI SANA YA MWANZO WA LIGI


Liverpool wamefanikiwa kiwafunga Arsenal 4-3 katika mechi kali sana ya kufungua msimu ndani ya Emirates...Arsenal ndio walioanza kuonyesha makeke mpaka kipindi cha 2 lakini baada ya hapo Liverpool walikuja na cheche kali za ziada...


Theo Walcott ndio aliyeanza kuona lango la Liverpool mapema dakika ya 31 baada ya Arsenal kukosa penalty...Wengine waliopata mabao ni Coutinho dakika ya 45+1 na 56, Lallana dakika ya 49, Sadio Mane dakika ya 63, Oxlade-Chambelain dakika ya 64 na Chambers dakika ya 75...


Arsenal inaonekana beki bado haiko sawasawa kabisa na Wenger inabidi atafute watu wenye uzoefu...Bofya hapa upate habari zaidi.

Thursday, 19 May 2016

EUROPA LEAGUE FINALS: SEVILLA MABINGWA TENA


Sevilla wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Europa League kwa kuwatandika Liverpool 3-1 jana usiku huko Basel...Liverpool walianza kucheza vizuri na hatimaye kabla ya mapumziko walipata bao safi kabisa kupitia Daniel Sturridge...Sturridge ni mchezaji wa kwanza kufunga bao Europa League/UEFA Cup toka Robbie Fowler afungee mwaka 2001...


Kipindi cha 2 Sevilla sijui waliambiwa nini na kocha maana walibadilisha game na kucheza kwa akili nyingi...Liverpool wakaanza kuchanganyikiwa na badae Klopp akamtoa Lallana lakini haikusaidia kwani Sevilla walikuwa wanacheza vizuri zaidi...


Katika mipira 4 iliyolenga goli mipira 3 ya Sevilla imeingia nyavuni...Wafungani wa Sevilla walikuwa Kevin Gameiro dakika ya 46 na Andujar Moreno mabao 2 dakika ya 64 na 70...


Sevilla wamefunga Sevilla wanachukua kombe kwa mara ya 3 mfululizo sasa...Bofya hapa upate habari zaidi.