Thursday, 30 June 2016

TFF: MECHI ZOTE ZA KIMATAIFA KUSIMAMIWA NA TFF KUANZIA SASA


TFF itasimamia mechi zote za kimataifa kuanzia sasa...TFF itasimamia kila kitu kinachihusu mechi za kimataifa kuanzia mapokezi ya timu za wageni,  usalama wa wachezaji mpaka kuratibu viingilio na uuzwaji wa tickets...Hii imekuja kutokana na Yanga kuruhusu mashabiki kuingia bure na kuzua balaa...Vyombo vya usalama vilipata kazi ya ziada baada ya watu kutaka kuingia uwanjani wakati kumejaa...Kanunu ya FIFA kifungu cha 67, CAF kifungu 59 na TFF kifungu cha 52 kinaruhusu Mamlaka husika kusimamia shughuli zote za machi za kimataifa...Bofya hapa upate habari zaidi.

YANGA: KAMATI YA MAADILI YAMTAKA JERRY MURO KUJIELEZA


Jerry Muro ameitwa na Kamati ya Maadili ya TFF ilikujieleza kutokana na vitendo vyake kabla ya mechi ya Yanga na TP Mazembe...Ni mara ya 3 Muro anaitwa mbele ya Kamati hiyo...Muro ni Mkuu wa Kitengo cha Habari Yanga...Muro anatakiwa kufika ofisi za TFF tarehe 2 au kama hatoweza atume mwakilishi kwa maandishi...Bofya hapa upate habari zaidi.

ARSENAL: THE GUNNERS WAMSAKA KIJANA HATARI KABISA GABRIEL BARBOSA KUTOKA BRAZIL


Arsenal bado wanaendelea kutafuta vifaa hatari kuimarisha safu ya mbele na sasa wameingia Brazil na huko kuna kijana anaitwa Gabriel Barbosa ambae ni hatari kabisa...

WIMBLEDON 2016: MARCUS WILLIS AMESEMA KUCHEZA NA ROGER FEDERER NI KAMA NDOTO


Marcus Willis ambae ni namba 772 duniani amesema kucheza na Roger Federer ilikuwa kama ndoto na alijisikia vizuri sana...Willis alitandikwa 6-0 6-3 6-4 na Roger Federer ambae ni namba 3 duniani...Willis alisema alikuwa na mipango ya kumchapa Federer na aliamini angeweza kumchapa lakini mkali Federer alimpeleka shule Willis na set ya kwanza tu Willis alitoka kapa...


Rankings mpya zikitoka Wimbledon atakuwa namba 416 kwa ukali duniani...Bofya hapa upate habari zaidi.

CHELSEA FC: MITCHY NDANI YA STAMFORD BRIDGE


Mchezaji hatari wa timu ya taifa ya Belgium na Marseille, Mitchy Batshuayi, tayari amekamilisha taratibu za usajili za kuingia Stamford Bridge...Mitchy amechukuliwa kwa dau la Pound milioni 33...Kwa sasa taratibu za kuangalia afya yake zimekamilika vizuri na yuko France tayari kucheza mechi za robo fainali zinazoanza leo usiku saa 4...Belgium wanatarajiwa kucheza kesho dhidi ya Wales...Bofya hapa upate bahari zaidi.

Wednesday, 29 June 2016

SAMUEL ETO'O: STRICKER SAMUEL ETO'O AFUNGA NDOA YA KIFAHARI ITALY




Striker hatari sana kutoka Cameroon na mwenye pesa nyingi zaidi ya wachezaji wengi Africa amefunga ndoa mpenzi wake wa siku nyingi Georgett Tra Lou...



Harusi hiyo ya mchezaji wa zamani wa Barcelona na misimu miwili alichezea nchini Italy akiwa na Inter Milan na Sampdoria ilifanyika Stezzano, Italy...



Baada ya kufunga ndoa watu wengi walifurika kanisani kumwona mke wa Eto'o...


Wageni waalikwa walikuwa wengi akiwemo mchezaji mwenzake wa zamani wa Barcelona Chareles Puyol...Bofya hapa upate habari zaidi.

CHELSEA: MITCHY WA BELGIUM KARIBU ANAINGIA STAMFORD BRIDGE


Chelsea wako karibu kumnyakua kifaa cha Belgium na Marseille Mitchy Batshuayi...Chelsea wako tayari kutoa Pounds milioni 33 kumchuku Mitchy...Timu nyingi zikiwemo West Ham united na Juventus wamepigwa chini kwa dau lao dogo na Crystal Palace walikubaliwa kwa milioni 31.6 lakini Chelsea wamapanda dau na kutoa offer ya milioni 33...Mitchy anaeza kuwa usajili wa kwanza wakati Conte anaingia darajani...Dogo huyo mwenye umri wa miaka 22 alipata mabao 17 msimu uliopita na alitoka benchi na kuifungia timu yake ya taifa Euro 2016...Bofya hapa upate habari zaidi.

WIMBLEDON 2016: RATIBA YA MECHI ZA LEO

Wimbledon

Men's Singles · 
P. Herbert
2nd Round
D. Dzumhur
Jun 29, 4:30 PM
30
A. Dolgopolov
2nd Round
D. Evans
Jun 29, 4:30 PM
N. Almagro
2nd Round
D. Istomin
Jun 29, 4:30 PM
28
S. Querrey
2nd Round
T. Bellucci
Jun 29, 3:30 PM

WIMBLEDON 2016: STAN WARWINKA KUCHUANA NA JUAN MARTIN DEL POTRO ROUND YA 2


Stan Wawrinka amefanikiwa kusogea round ya 2 ya michuano mikubwa sana ya Wimbledon huko England baada ya kumchapa dogo kutoka America Taylor Fritz...Wawrinka ambae ni namba 4 Switzerland amemchapa dogo Fritz mwenye umri wa miaka 18 7-6 (7-4) 6-1 6-7 (2-7) 6-4...Wawrinka sasa atakutana na Juan Martin Del Potro round ya 2...Del Potro anayetokea Argentina aliwahi kushinda US Open ya mwaka 2009 amefanikiwa kumtoa Stephane Robert 6-1 7-5 6-0...Bofya hapa upate habari zaidi.

CAF CONFEDERATION CUP 2016: YANGA YAZAMISHWA NA MERVEILLE BOPE


Ndoto za Young Africans au maarufu kwa jina la Yanga jana liishia ukingoni baada ya kufungwa bao pekee na Merveille Bope...Bao hili la TP Mazembe liliingia mnamo dakika ya 70 na ushee hivi mbele ya mashabiki kibao waliopata nafasi ya kuangalia mechi bure...Mechi nyigine ya yanga itakuwa na Madeama ya Ghana kati ya tarehe 15, 16 au 17...


Ushindi dhidi ya Madeama nyumbani na ushindi dhidi ya Yanga umeipa TP Mazambe wana wa Lubumbashi points 6 na kuongoza Group A...Ni ushindi wa kwanza wa nje wa TP Mazembe mwaka huu katika michuano ya Caf...Bofya hapa upate habari zaidi.

CAF CONFEDERATION CUP: AL AHLY HOI KWA ASEC MIMOSAS


Asec Mimosas ya Abdijan wamefanikiwa kuwachapa mabingwa wa Egypt Al Ahly 2-1 nyumbani ndani ya Borg El Arab...Mabao hayo yametoka kwa Yannick Zakri na Armand Nianke...Al Ahly wametoka kunyakua ubingwa kutoka kwa Zamalek sasa wana kazi ya ziada maana hawakutegemea kuchapwa... Bofya hapa upate habari zaidi.

Tuesday, 28 June 2016

LIVERPOOL: MANE ATOKA KWA DAKTARI WA LIVERPOOL AKIONYESHA ISHARA YA MAMBO YAKO POA


Sadio Mane amemaliza uchunguzi wa daktari na alivyokuwa anatoka akaonyesha idhara ya dole gumba kuwa mambo yako shwari...Mane yuko tayari kuichangamsha timu ya Liverpool msimu mpya...Southampton wametengeneza pesa nyingi kwenye dili la Mane...Dili hili ni Pounds milioni 30...Ni dili la 3 kwa Liverpool la bei ya juu sana ukiacha Andy Carol na Christan Benteke...Mane mwenye umri wa miaka 24 aliingia Southampton akitokea timu ya Red Bull Salzburg kwa Pound milioni 11...Bofya hapa upate habari zaidi.

EURO 2016: RATIBA YA MECHI ZA ROBO FAINALI (GMT)

  •   

    POLPOR
    Stade Vélodrome, Marseille
  •   

    WALBEL
    Stade Pierre-Mauroy, Lille
  •   

    GERITA
    Matmut Atlantique, Bordeaux
  •   

    FRAICE
    Stade de France, Paris