Showing posts with label Moise Katumbi. Show all posts
Showing posts with label Moise Katumbi. Show all posts

Wednesday, 29 June 2016

CAF CONFEDERATION CUP 2016: YANGA YAZAMISHWA NA MERVEILLE BOPE


Ndoto za Young Africans au maarufu kwa jina la Yanga jana liishia ukingoni baada ya kufungwa bao pekee na Merveille Bope...Bao hili la TP Mazembe liliingia mnamo dakika ya 70 na ushee hivi mbele ya mashabiki kibao waliopata nafasi ya kuangalia mechi bure...Mechi nyigine ya yanga itakuwa na Madeama ya Ghana kati ya tarehe 15, 16 au 17...


Ushindi dhidi ya Madeama nyumbani na ushindi dhidi ya Yanga umeipa TP Mazambe wana wa Lubumbashi points 6 na kuongoza Group A...Ni ushindi wa kwanza wa nje wa TP Mazembe mwaka huu katika michuano ya Caf...Bofya hapa upate habari zaidi.

Tuesday, 26 January 2016

MBWANA SAMATTA: TAJIRI MOSE KATUMBI AKUBALI SAMATTA KWENDA GENK



Hatimae mwanasoka bora Afrika Mbwana Samatta amepata upenyo wa kwenda kucheza soka Ulaya ya Tajiri mkubwa sana Congo na mmiliki wa TP Mazembe Moise Katumbi kukubali offer ya KRC Genk...KRC Genk ni timu ya premiership ya Ubelgiji...Genk ni kati ya timu kubwa Ubelgiji ambayo umecheza UEFA Champions League mara 4 na EUROPA mara 6...


Hapo awali Katumbi aligoma kumwachia Samatta kwasababu pesa ya transfer ilikuwa ndogo lakini sasa amebariki move na sasa Samatta anajiandaa kwenda Ubelgiji muda wowote kuanzia sasa...Bofya hapa upate habari zaidi.