Saturday, 30 January 2016

K.R.C. GENK: MBWANA SAMATTA AINGIA RASMI GENK



Mbwana Samatta amesajiliwa rasmi na timu ya K.R.C. Genk ambayo iko nafasi ya 6 sasa kwenye Belgian Pro League...Samatta ni mwanasoka bora Afrika na Tanzania tunajivunia kuwa na kifaa kikali sana...Samatta ametokea timu ya TP Mazembe na huko alikuwa mchezaji bora...Amewahi kuichezea Simba hapo nyuma...Kila la heri Mbwana Samatta katika maisha ya soka Ulaya...Bofya hapa upate habari zaidi.

CHELSEA: PATO AINGIA DARAJINI RASMI KWA MKOPO



Brazilian stiker Alexandre Pato katia timu darajani....Pato kaingia kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu...Kwa uzoefu amechezea nchi yake mara 27 na kufifungia mabao 10...Kwa hali Chelsea ilipo Pato atawasaidia angalau waweze kumaliza nafasi nzuri msimu huu...Bofya hapa upate habari zaidi.

Friday, 29 January 2016

ARSENAL: VIJANA WAWILI HATARI SANA KUTOKA DIAMOND FOOTBALL ACADEMY NIGERIA MBIONI KUINGIA EMIRATES


Arsenal imeshinda mbio za kuwanyakua vijana hatari sana kutoka Diamond Football Academy nchini Nigeria, Kelechi Nwakali na Samuel Chukwuezi, kwa pounds za Uingereze milioni 3...Arsenal katika mbio hizo wameweza kuwatoa Manchester City na Bayern Munich...Arsenal walianza kuwatafuta vijana hawa machachari mwaka jana kwenye mashindano ya World Cup ya  U-17 nchini Chile na katika michuano hiyo Nwakali alikuwa Captain na mchezaji bora na Chukwuezi alipachika mabao 3 na assist 3...Bofya hapa upate habari zaidi.

NEMANJA VIDIC: TOP MANCHESTER UNITED PLAYER RETIRES



Nemanja Vidic is a player who was very instrumental in the success of Manchester United has decided to call it quits.

FA CUP: RATIBA YA MECHI ZA JUMAMOSI (GMT)


AUSTRALIAN OPEN 2016: DJOKOVIC AMCHAPA FEDERER AINGIA FAINALI



Novak Djokovic amefanikiwa kuingia fainali za Australian Open baada ya kumchapa mkongwe Roger Federer...Djokovic alianza seti mbili za mwanzo kwa nguvu na kuzidiwa seti ya 3 na badae akapambana na kushinda seti ya 4...Djokovic alishinda kwa 6-1 6-2 3-6 6-3 na sasa anasubiri kucheza na Andy Murray au Raonic...Bofya hapa upate habari zaidi.

FA CUP: RATIBA YA MECHI YA LEO (GMT)

YANGA: MALINZI TELLS YANGA TO SET EARLY ELECTIONS



Rais of the Tanzania Football Federation (TFF), Jamal Malinzi, has told  Yanga to set their elections as early as possible.

Thursday, 28 January 2016

NATIONAL RALLY CHAMPIONSHIP: RALLY YA TANGA YAFUTWA



Rally ambayo ilikuwa ifungue msimu imefutwa...Chama cha magari nchini Automobile Association of Tanzania (AAT) kimetangaza kuwa Rally ya Tanga imefutwa kutokana na uongozi wa Rally Tanga haujajipanga vizuri na haukufuata masharti ya chama hicho...Rais wa AAT, Nizar Jivani, amesema Tanga wanaweza kuandaa Club Rally na watapata ushirikiano wote  na sasa National Rally itaanzia Moshi, Kilimanjaro March...Rais wa chama cha Rally Kilimanjaro, Fahim Aloo, amesema wako tayari kuwa wenyeji wa mashindano hayo na maadalizi yamepamba moto...Bofya hapa upate habari zaidi.

EPL: MSIMAMO WA LIGI MPAKA SASA

Position Team Played Goal Diff Points
 1 Leicester 23 16 47
 2 Man City 23 22 44
 3 Arsenal 23 15 44
 4 Tottenham 23 22 42
 5 Man Utd 23 7 37
 6 West Ham 23 8 36
 7 Liverpool 23 -2 34
 8 Southampton 23 8 33
 9 Stoke 23 -1 33
 10 Watford 23 1 32
 11 Crystal Palace 23 -3 31
 12 Everton 23 6 29
 13 Chelsea 23 -2 28
 14 West Brom 23 -8 28
 15 Swansea 23 -9 25
 16 Bournemouth 23 -11 25
 17 Norwich 23 -15 23
 18 Newcastle 23 -16 21
 19 Sunderland 23 -18 19
 20 Aston Villa 23 -20 13

COPA DEL REY: BARCELONA NDANI YA NUSU FAINALI



Bacelona wanafukuzia vikombe 5 msimu na kimoja wapo wanachokitaka ni Copa del Rey...Athletic Bilbao walichapwa 3-1 na kuwaingiza Barca nusu fainali...Barca walishangazwa mapema baada ya Inaki Williams kupachika bao dakika ya 12...Suarez alisawazisha mapema kipindi cha 2 na mabao mengine walikuwa badae kwenye dakika ya 81 na 90+1 kupitia Pique na Neymar...Bofya hapa upate habari zaidi.

Wednesday, 27 January 2016

YANGA: UCHAGUZI MAANDALIZI YAANZA


Club ya Yanga sasa iko mbioni kutayarisha uchaguzi wa club hiyo...Msemaji wa Yanga, Jerry Muro, amesema mambo sasa yameiva baada ya Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, kumchagua mwanasheria Mapande kusimamia kamati ya uchaguzi ili iweze kuandaa uchaguzi baada ya hiyo nafasi kuachwa wazi na mwanasheria Alex Mgongolwa...Mgongolwa alisema anaachia ngazi kwasababu anataka kupata muda wa kukaa na familia...Yusuf Manji amesema atasimama kutetea kiti cha uenyekiti na amesema watu wengine wajitokeze...Bofya hapa upate habari zaidi.

CAPITAL ONE CUP 2016: LIVERPOOL YA KLOPP NDANI YA FAINALI


Liverpool imefanikiwa kuingia fainali ya League Cup chini ya uongozi wa Jurgen Klopp...Liverpool walifanikiwa kuchinda kupitia matuta baada ya kufungwa 0-1 na Stoke City...


Pamoja na kipa wa Liverpool, Simon Mignolet, kulaumiwa sana kipa huyo ndiye aliyekuwa staa baada ya kupangua penalty za Peter Crouch na Marc Muniesa...Bofya hapa upate habari zaidi.

AUSTRALIAN OPEN 2016: JOHHANA KONTA NA ANDY MURRAY WAINGIA NUSU FAINALI



Uingereza kwa mara ya kwanza toka mwaka 1977 inawachezaji wawili ndani ya nusu fainali...Johanna Konta na Andy Murray walifanikiwa kuiingia nusu fainali ya Australian Open baada ya kuwachapa Zhang Shuai kutoka China na David Ferrer kutoka Spain...


Mechi nyingine Raonic alifanikiwa kuingia nusu fainali kwa mara ya kwanza alivyomchapa Gael Monfils 6-3 3-6 6-3 6-4...Bofya hapa upate habari zaidi.

Tuesday, 26 January 2016

SIMBA SPORTS CLUB: KOCHA KERR ABWAGA MANYANGA KWA KUACHA BARUA


Kocha wa Simba Sports Club Dylan Kerr ameandika barua ndefu kwa mashabiki na waandishi wa habari juu ya sababu za kusepa...Kwa ujumla barua hiyo ni ndefu na inashukuru sana mashabiki wa Simba kwa upendo wao kwa timu na pia inalaumu uongozi kwa kuingilia masuala ya ukocha bila uelewa wa kitaalam...Kerr amesema bodi haina hata mtu mmoja mwenye qualifications za Caf  na pia wajumbe kadhaa wa bodi wanairudisha timu nyuma sana...Malalamiko kibao ameyaweka kwenye hiyo barua ambayo kwa ujumla ni kuiaga club ya Simba na mashabiki wake na kutoa mwongozo wa kurekebisha mambo...Bofya hapa upate habari zaidi.

MBWANA SAMATTA: TAJIRI MOSE KATUMBI AKUBALI SAMATTA KWENDA GENK



Hatimae mwanasoka bora Afrika Mbwana Samatta amepata upenyo wa kwenda kucheza soka Ulaya ya Tajiri mkubwa sana Congo na mmiliki wa TP Mazembe Moise Katumbi kukubali offer ya KRC Genk...KRC Genk ni timu ya premiership ya Ubelgiji...Genk ni kati ya timu kubwa Ubelgiji ambayo umecheza UEFA Champions League mara 4 na EUROPA mara 6...


Hapo awali Katumbi aligoma kumwachia Samatta kwasababu pesa ya transfer ilikuwa ndogo lakini sasa amebariki move na sasa Samatta anajiandaa kwenda Ubelgiji muda wowote kuanzia sasa...Bofya hapa upate habari zaidi.

AUSTRALIAN OPEN 2016: SERENA WILLIAMS AMCHAPA TENA SHARAPOVA



Serena Williams ameonyesha ukali wake baada ya kumchapa tena Maria Sharapova....Serena amemchapa Sharapova kwa mara ya 18 mfululizo na kuingia nusu fainali ya michuano mikali sana ya Australian Open huko Melbourne...Serena ambae ni namba 1 duniani alimchapa Sharapova 6-4 6-1 na sasa anafukuzia Grang Slam ya 22...Katika mechi nyingine Roger Federer alifanikiwa kumchapa Tomas Berdych 7-6 (7-4) 6-2 6-4...Bofya hapa upate habari zaidi.

CHELSEA: RAMIRES MBIONI KUTINGACHINA KWA MILIONI 25 POUNDS



Jiangsu Suning tumu ya China itamchukua Brazilian international  Ramires kwa dau kubwa la milioni 25 pounds...Suning walichukua Chinese Cup mwaka 2015 na walimaliza premiership yao wa 9...Ramires alitokea Benfica kwa milioni 17 pounds...Bofya hapa upate habari zaidi.

Monday, 25 January 2016

VPL: MSIMAMO WA WANAOONGOZA LIGI

Pos Club P GD PTS
1 Young Africans SC 15 31 39
2 Azam FC 15 20 39
3 Simba SC 15 14 33
4 Mtibwa Sugar FC 15 9 28
5 Stand United 15 5 28
6 Tanzania Prisons 15 1 27
7 Mwadui FC 15 4 25
8 Toto African 15 -6 17

NFL: DENVER BRONCOS KUKUTANA NA CAROLINA PANTHERS SUPER BOWL 50



Denver Broncos waingia tena fainali ya NFL au kwa jina maarufu sana duniani la Super Bowl baada ya kuwachapa wakongwe New England Patriots 20-18...Kwa upande mwingine Carolina Panthers wakiongozwa na Cam Newton waliwachapa Arizona Cardinals 49-15...



Quarterback wa Broncos MVP mara 5 mkongwe Peyton Manning atakuwa mchezaji mwenye umri mkubwa kuliko wote akiwa na umri wa miaka 39...Super Bowl 50 itachezwa February 8 ndani ya uwanja wa  Levi's ndani ya jiji la San Fransisco saa 8 na dakika 20 usiku muda wa East Africa...Bofya hapa upate habari zaidi.

EPL: MSIMAMO WA LIGI MPAKA SASA

Position Team Played Goal Dif. Points
 1 Leicester 23 16 47
 2 Man City 23 22 44
 3 Arsenal 23 15 44
 4 Tottenham 23 22 42
 5 Man Utd 23 7 37
 6 West Ham 23 8 36
 7 Liverpool 23 -2 34
 8 Southampton 23 8 33
 9 Stoke 23 -1 33
 10 Watford 23 1 32
 11 Crystal Palace 23 -3 31
 12 Everton 23 6 29
 13 Chelsea 23 -2 28
 14 West Brom 23 -8 28
 15 Swansea 23 -9 25
 16 Bournemouth 23 -11 25
 17 Norwich 23 -15 23
 18 Newcastle 23 -16 21
 19 Sunderland 23 -18 19
 20 Aston Villa 23 -20 13

EPL: CHELSEA YAPONEA KUPITIA ARSENAL YA WATU 10


Kutokana na kadi nyekundu aliyepewa Mertersacker wa Arsenal mapema kwenye dakika ya 18 Chelsea kupitia Diego Costa walishinda kwa bao hilo pekee kutokana na uzembe wa mabeki wa Arsenal...Arsenal walicheza vizuri kama hakuna mtu nje na walikosa mabao kadhaa lakini pamoja na hayo Chelsea nao walikomaa na kudhibiti mianya ya mabao...Mchezaji wa Chelsea Willian Borges da Silva ndie pekee aliyecheza vizuri kwa upande wa Chelsea...Arsene Wenger alifanya sub baada tu ya ile kadi nyekundu kwa kumtoa Giroud lakini wadau wa mpira waliona hiyo move kama ni kosa ingawa Wenger alikuwa anataka kuimarisha beki na alikuwa na sababu zake pia...Bofya hapa upate habari zaidi.

Sunday, 24 January 2016

MANCHESTER UNITED: VICTOR VALDEZ AINGIA STANDARD LIEGE


Spanish international kipa Victor Valdez ameingia timu ya Ubelgiji ya Standard Liege kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu...Valdes alikuwa na matatizo na kocha wa Man U Van Gaal na kukaa benchi muda mrefu sana...Kisa eti Vaaldes aligoma kucheza mechi ya mazoezi ndio maana Van Gaal alimweka benchi lakini kuna mambo mengi yalichangia kocha huyo kuchukua hatua kali...Bofya hapa upate habari zaidi.

EPL: PATA 11 YA EVERTON NA SWANSEA KATIKA GAME YA LEO

Pata 11 ya Everton kabla ya game ya leo dhidi ya Swansea...Hapo chini ni 11 ya Swanswa...Mechi inategemewa kuwa kali sana usikose kuangalia....Bofya hapa upate habari zaidi.

CHAN 2016: ZAMBIA YAFUZU KUINGIA ROBO FAINALI



Zambia imefuzu kuingia  robo fainali ya African Nations Championship (CHAN) baada ya kuichapa Uganda 1-0 katika Goup D...

EPL: RATIBA YA MECHI ZA LEO (GMT)

AUSTRALIAN OPEN 2016: DJOKOVIC AFANYA MAKOSA 100 LAKINI ASHINDA


Gilles Simon karibu amtoe namba 1 duniani Novak Djokovic lakini Djokovic aliweza kushinda 6-3 6-7 (1-7) 6-4 4-6 6-3...Katika uwanja wa Rod Laver mechi ilichukua masaa 4 na dakika 32 Djokovic akifanya makosa 100 au kwa lugha nyingine 100 unforced errors ambazo zingemfanya achapwe lakini aliweza kupata mwanga na kushinda...Djokovic sasa kaingia 8 bora na atapambana na Kei Nishikori kutoka Japan...Bofya hapa upate habari zaidi.

Saturday, 23 January 2016

EPL: MSIMAMO WA LIGI MPAKA SASA

PositionTeamPlayedGoal Dif. Points
1Leicester 231647
2Arsenal 221644
3Man City 232143
4Tottenham 232242
5West Ham 23938
6Man Utd 23737
7Liverpool 23-234
8Southampton 23833
9Stoke 23-133
10Watford 23132
11Crystal Palace 23-331
12Everton 22729
13West Brom 23-828
14Chelsea 22-325
15Bournemouth 23-1125
16Norwich 23-1523
17Swansea 22-1022
18Newcastle 23-1621
19Sunderland 23-1819
20Aston Villa 23-2013

EPL: LIVERPOOL YACHOMOKA MWISHONI KABISA KATIKA MECHI KALI DHIDI YA NORWICH


Liverpool FC kupitia Adam Lalana wamechomoka dakika kama ya 95 vile baada ya kuchapa mkwaju hatari...Liverpool wameshinda 5-4 na sasa wanaweza kupumua maana mechi ilikuwa kama danadana na timu zote zilijitahidi sana na pia kuna wakati walichemsha...Bao la Lalana lilimfanya kocha Jurgen Klopp kuvunja miwani yake alipokuwa anashangilia bao la 5 na la mwisho...Liverpool wameonyesha tena kuwa wao ni wataalam wa kugeuza mambo yakiwa yameenda kombo...Bofya hapa upate habari Zaidi.

EPL: RATIBA YA MECHI ZA LEO (GMT)

AUSTRALIAN OPEN 2016: NAMBA 3 DUNIANI NJE




Australian Open imeanza kupamba moto kwani kutolewa kwa wakongwe sio jambo la kawaida...Namba 3 duniani, Gabrine Muguruza, kafyekwa na namba 48 duniani Barbora Strykova 6-3 6-2...Bofya hapa upate habari zaidi.