Showing posts with label Super Bowl 50. Show all posts
Showing posts with label Super Bowl 50. Show all posts

Friday, 5 February 2016

SUPER BOWL 50: SNOOP DOGG AWAFURAHISHA WACHEZAJI WA BRONCOS NA PANTHERS KWENYE MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI



Msanii maarufu wa miondoko ya Hip-Hop, Snoop Dogg, amewafurahisha sana wachezaji wa timu mbili kubwa ambazo zimefika fainali ya ligi ya NFL, Denver Broncos na Carolina Panthers...


Snoop Dogg aliibuka kwenya mkutano wa timu hizo 2 na waandishi wa habari na kuweza kuwauliza maswahi kadhaa wachezaji na pia kuwatania kidogo na kupiga nao picha...


Snoop aliwatakia heri timu zote katika fainali itayofanyika Jumapili ijayo...Bofya hapa upate habari zaidi.

Monday, 25 January 2016

NFL: DENVER BRONCOS KUKUTANA NA CAROLINA PANTHERS SUPER BOWL 50



Denver Broncos waingia tena fainali ya NFL au kwa jina maarufu sana duniani la Super Bowl baada ya kuwachapa wakongwe New England Patriots 20-18...Kwa upande mwingine Carolina Panthers wakiongozwa na Cam Newton waliwachapa Arizona Cardinals 49-15...



Quarterback wa Broncos MVP mara 5 mkongwe Peyton Manning atakuwa mchezaji mwenye umri mkubwa kuliko wote akiwa na umri wa miaka 39...Super Bowl 50 itachezwa February 8 ndani ya uwanja wa  Levi's ndani ya jiji la San Fransisco saa 8 na dakika 20 usiku muda wa East Africa...Bofya hapa upate habari zaidi.