Wednesday 13 January 2016

ENGLAND: GARY LINEKER ACHANA NA MKE WAKE


Mchezaji maarufu wa England wa zamani na anayeshikilia rekodi ya mabao kwenye fainali za FIFA World Cup, Gary Lineker, ameachana na mke wake Danielle...Kisa ni kutokana na kutoelewana katika kuongeza watoto...Mke anataka watoto lakini Gary anasema hatake umri umeenda sana hawezi kuwa baba tena...Kwa mwaka sasa hawakai pamoja na ndoa yao ilidumu kwa miaka 6...Lineker na Danielle ambae ni model wa nguo za ndani za wanawake walikutanishwa na mshkaji wao...Wameamua kuachana bila ugomvi na Lineker mwenye utajiri wa zaidi ya milioni 20 atamkatia kidogo pesa mke wake...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment