Wednesday 18 June 2014

WORLD CUP 2014: FRANCISCO GUILLERMO OCHOA AWA KINARA WA GAME YA BRAZIL NA MEXICO



Guillermo Ochoa kipa wa Mexico amekuwa kinara wa mechi kali sana ambayo mpaka sasa tulikuwa hatujawahi kuona mechi kali kama hii ya Brazil na Mexico...

Ochoa ambae alipangua mabao mengi kutoka kwa Brazil alitunukiwa 'Man of the Match'.



Brazil kiukweli walitolewa jasho sana na Mexico kuanzia katikati ya mchezo mpaka mwishoni.

Timu zote zilicheza vizuri sana.

Mashambulizi mengi sana.

Lakini kama watu walivyotegemea kwamba Brazil walitakiwa kushinda haikuwa hivyo kutokana na mtu mmoja anaitwa Ochoa.


Kipa huyu aliwakosesha ushindi Brazil na hii haijawahi kutokea toka mwaka 1978 Brazil wameshidwa kushind mechi ya 2 ya World Cup.



Neymar alikataliwa kufunga goli kali na Ochoa ambalo linafananishwa na Pele alivyokatakiwa na kipa Gordon Banks World Cup ya 1970.

Hii ni mechi ya pili sasa kwenye World Cup hii kutoka sare bila kufungana...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment