Sunday 8 June 2014

BOXING: COTTO AMSMAMISHA MARTINEZ ROUND YA 10



Miguel Cotto ameweka historia ya Boxing baada ya kumchapa kisawsawa Sergio Martinez kwa TKO ya round ya 10.





Katika ukumbi wa Madison Square Garden ambao ulijaa watu kama 21,000 na wengi kutoka Puerto Rico walifanikiwa kuona historia kwani ni mtu pekee kutoka hicho kisiwa kushinda ubingwa wa dunia kwenye uzito tofauti mara 4.


Uzito aliochukua ubingwa wa dunia ni middleweight, junior middleweight, welterweight na junior welterweight.

Cotto alikuwa imara toka mwanzo na alimwangusha Martinez mara 3 round ya mwanzo.



Martinez alishushwa mara ya kwanza na left-hook, m
ara ya 2 na konde la kulia.

Mara ya 3 alichapwa kwenye mwili.


Kocha maarufu sana Freddy Roach amemsifi Miguel Cotto na kusema alistahili kuweka historia...Bofya hapa upate mambo zaidi...

No comments:

Post a Comment