Sunday, 22 June 2014

WORLD CUP 2014: GHANA YAIKIMBIZA GERMANY


Katika hii World Cup tumeona historia zikivunjwa na pia tukaona timu ambazo hazikutegemewa kufanya vizuri zikin'gara...

Jana usiku katika uwanja wa Fortaleza tuliona Ghana ikiikimbiza Ujerumani ambayo ni timu wadau wanasema ni bora kuliko zote.

Ghana waliwavuia uvivu Ujerumani na kucheza mpira wa ukweli.

Baada ya Mario Goetze kupachika bao dakika y 51 Ghana walicheza mpira safi na baada ya muda si mrefu Adrew Ayew alipachika bao la kichwa.


Sulley Muntari nae alimpa pande Asamoah Gyan ambaye hakufanya makosa na nyavu zikatikisika.

Substitute wa Ujerumani Miroslav Klose dakika ya 71 alisawazisha kwa goli gumu na pia ilikuwa maya yake ya kwanza kugusa mpira toka aingizwe.


Klose sasa amemfikia rekodi Ronaldo kwa kuwa mtu aliyefunga magoli mengi World Cup.

Pia Klose ni kati ya wachezaji wa tatu tu duniani ambao wamewahi kufunga goli katika Wold Cup 4 tofauti wengine ni Pele na Uwe Seeler.

Asamoah Gyan ni mwafrika wa kwanza kupachika bao katika World Cup 3 tofauti...Bofya hapa upate kujua kwanini hii mechi ilikuwa kali kuliko zote....

No comments:

Post a Comment