Saturday 28 June 2014

WORLD CUP 2014: BRAZIL YAINGIA 8 BORA


Brazil imefanikiwa kuingia 8 bora baada ya kuitoa Chile kwenye matuta...Brazil walicheza vizuri lakini sio vizuri kama Brazil tunavyowajua...Chile walicheza vizuri sana na kuikimbiza Brazil mara kwa mara...David Luiz aliipatia nchi yake bao dakika ya 18 na pia ni bao lake la kwanza kwenye mechi ya kimataifa...


Alexis Sanchez dogo anayechezea Barca alipachika goli zuri kushoto mwa goli la Brazil dakika ya 32...Refa aliwanyima Brazil goli baada ya Hulk kupachika bao dakika ya 55 ilionekana hakushika mpira bali ameonewa...Dakika za nyongeza bado walikuwa 1-1...Dakina za nyongeza wote walivuta kasi ya kushambuliana lakini hakuna aliyeweza kuona lango la mwenzio...


Julio kipa wa Brazil alikuwa makini kwa kupangua penalty 2 kali...Mwisho Brazil walishinda 3-2 kwenye matuta...

No comments:

Post a Comment