Friday 13 June 2014

WORLD CUP 2014: BRAZIL YASHINDA 3-1 KWA SHIDA

 
Timu zikiingia uwanjani na watoto

Brazil ilifanikiwa kushinda mechi yake ya kwanza dhidi ya Croatia 3-1 katika uwanja wa Arena de Sao Paulo...Croatia ndio walianza kupata goli la bure baada ya kusaidiwa na Marcelo ambae alijifunga dakika ya 11...Dogo Neymar alisawazisha dakika ya 29...Croatia walikuwa wanacheza mpira wa uhakuka na Brazil walipoteza utaalam wao mwanzoni lakini waliupata baadae...Kocha wa Croatia Niko Kovac alichukizwa sana na maamuzi yaliyo kuwa yanatolewa na mwamuzi kutoka Japan Yuishi Nichimura...Mnamo dakika ya 70 Kovac alikasirika tena baada ya huyo refa kutoa penalty ya bure kabisa...
 
Neymar akishangilia goli...

Neymar ndio aliye piga penalty ambayo kipa aliifuata lakini ilikuwa na nguvu ikaingia nyavuni...Dogo Oscar alifunga goli zuri sana pekeyake dakika za mwishoni...Ushindi ni muhimu na sasa Brazil wamepata pointi 3...Usikose kuangalia mechi za leo....Mexico vs. Cameroon, Spain vs. Netherlands na Chile vs. Australia... 

No comments:

Post a Comment