Monday 9 June 2014

F1: RICCIARDO ASHINDA GP YA CANADA KWA STYLE


Ricciardo ameyakua kombe la GP huko Canada baada ya kumpita Nico Rosberg wa Mercedes mwishoni wakati zimebaki laps 2...Ricciardo ambaye yuko timu ya Reb Bull alijitahidi sana baada ya Lewis Hamilton kutoka kutokana na matatizo ya brakes...Sasa Hamilton yuko nyuma ya Nico Rosberg kwa pointi 22...Mashindano haya ya Canada yalikuwa makali sana toka kona ya kwanza mpaka mwisho...Tumeona Massa akipata ajali mbaya sana ambayo ilisababishwa na Sergio Perez wakati wanashindana....
 
Ajali ya Massa iliyosababishwa na Perez

Perez alimgonga Massa na gari la Massa likakosa mwelekeo na kugonga kingo za pembeni...Perez amepewa adhabu na uongozi wa F1 kutokana na ajali hiyo...Massa na Perez walipelekwa hospitalini lakini wanaendelea vizuri sasa baada ya kuachiwa huru na madaktari....Bofya hapa upate habari zaidi...

No comments:

Post a Comment