Friday 13 June 2014

WORLD CUP 2014: CAMEROON YACHPWA NA MEXICO



Cameroon imeanza vibaya michuano ya Wold Cup baada ya kuchapwa na Mexico bao 1 kwa 0 hapo Estadios des Dunas katika mji wa Natal...Mechi ya leo ilichezwa wakati mvua yingi nikinyesha mwanzo mwisho...



Cameroon ikiongozwa na Samuel Eto ilianza kwa kushambuliwa sana na Mexico na kukoswa mara nyingi kwani mshika kibendera alikuwa anawadaka Mexico kwa kuotea mara nyingi na pia kuna wakati refa aliwaonea Mexico mara 2...Cameroon walijitahi kuamka na kuwapelekea mpira Mexico lakini ilikuwa ngumu...Pia kulikuwa na rafu nyingi lakini refa alikuwa hatoi kadi kabisa mpaka mwishoni mwa kipindi cha pili...



Kipa wa Cameroon alijitahidi sana kupangua na kurukia mipira...Kuna kipindi Eto aligonga mwamba na akabaki anashangaa tu...Orilbe Peralta ndio aliwatoa Mexico kwa bao ambalo lilisababishwa na mabeki wa Cameroon kulala...Benoit Assou-Ekotto ndio mchezaji aliyejituma sana game ya leo...Bofya hapa usome zaidi...

No comments:

Post a Comment