Monday, 30 June 2014

WORLD CUP 2014: UTANI WA KLM WAZUA UTATA KWENYE TWITTER

Shirika la ndege la Netherlands, Royal Dutch Airlines au KLM, wamezua utata mkubwa sana kwa kuweka picha ambayo iliwatibua mashabiki wa Mexico na wadau wengine...Shirika la ndege la Mexico AeroMexico nao wakajibu kwenye twitter yao...Mambo ya World Cup mwaka huu matamu na machungu...Hii ni World Cup ya aina yake na imejaa furaha sana...Hebu cheki hapo chini KLM na AeroMexico wakitaniana...


Kwanza walianza KLM...na kusema Adios Amigos!


Wakajibu AeroMexico...Tunashukuru kwa mashindano haya makubwa, tunafuraha na tunasubiriwa nyumbani....




Bofya hapa usome watu walivyo jibu hizo tweets...

WORLD CUP 2014: NETHERLANDS YASHINDA KWA TABU SANA

Giovani dos Santos akipachika bao

Netherlands ilishind amechi yake dhidi ya Mexico kwa shida sana na pia imeonekana walibebwa na refa baada ya Robben kujirusha ndani ya 18...Mechi ilikuwa kali sana kwani Mexico waliwakimbiza sana Netherlands na hatimaye kupata bao dakika ya 48...dos Santos ndiye aliyepachika bao safi...Netherlands nao hawakuwa vilza kwani nao walijitahidi sana hasa Robben na Super-Sub Klaas...
 
Sneijder akiwaokoa Netherlnds

Netherlands waliweza kusawazisha dakika ya 88 kupitia kwa Sneijder...Klaas aliweza kuingia dakika ya 76 na kuisaidia sana Netherlands kwani walizidiwa...Mwishoni Netherlands walichangamka kidogo na ndipo Robben alipojirusha na refa akagawa penalty na kadi...Netherlands wanajua hiyo mechi hawakustahili ushindi...Bofya hapa usome zaidi...

WORLD CUP 2014: COSTA RICA WASONGA MBELE

 
Bryan Ruiz akipachika bao

Costa Rica imesonga mbele kwenye michuano ya World Cup baada ya kuichapa Greece 5-3 kwenye matuta...Costa Rica walicheza vizuri na pia walikuwa chini mtu mmoja kwa zaidi ya saa moja baada ya Oscar Duarte kutolewa...Bao lilipatikana dakika ya 52 baada ya Bryan Ruiz kupachika wavuni...Mwisho kabisa wakati dakika zinayoyoma Papastathopoulos (hawa jamaa na majina yao unaweza kupaliwa wakati unayataja) alisawazisha...
 
Kipa wa Costa Rica Keylor Navas akipangua penalty

Baaa ya hapo ilikuwa ni matuta tu...Game haikuwa kali sana kama ile ya Netherlands na Mexico lakini kwa kuwa walifika mpaka matuta ilitosa kwa mashabiki na watazamaji kwa ujumla...Bofya hapa upate habari zaidi...

Saturday, 28 June 2014

WORLD CUP 2014: BRAZIL YAINGIA 8 BORA


Brazil imefanikiwa kuingia 8 bora baada ya kuitoa Chile kwenye matuta...Brazil walicheza vizuri lakini sio vizuri kama Brazil tunavyowajua...Chile walicheza vizuri sana na kuikimbiza Brazil mara kwa mara...David Luiz aliipatia nchi yake bao dakika ya 18 na pia ni bao lake la kwanza kwenye mechi ya kimataifa...


Alexis Sanchez dogo anayechezea Barca alipachika goli zuri kushoto mwa goli la Brazil dakika ya 32...Refa aliwanyima Brazil goli baada ya Hulk kupachika bao dakika ya 55 ilionekana hakushika mpira bali ameonewa...Dakika za nyongeza bado walikuwa 1-1...Dakina za nyongeza wote walivuta kasi ya kushambuliana lakini hakuna aliyeweza kuona lango la mwenzio...


Julio kipa wa Brazil alikuwa makini kwa kupangua penalty 2 kali...Mwisho Brazil walishinda 3-2 kwenye matuta...

WIMBLEDON: RATIBA YA LEO




 Saturday, 28 June 2014

Centre Court (13:00 UK start)

Seed Player
Player Seed Competition
  Kukushkin (Kaz) v Nadal (Spa) Men's Singles
  Riske (US) v Sharapova (Rus) Women's Singles
  Giraldo (Col) v Federer (Sui) Men's Singles

No.1 Court (13:00 UK start)

Seed Player
Player Seed Competition
S Williams (US) v Cornet (Fra) 25  Women's Singles
11  Ivanovic (Ser) v Lisicki (Ger) 19  Women's Singles
Wawrinka (Sui) v Istomin (Uzb)   Men's Singles

YANGA: MAXIMO ASEMA ATAIWEKA YANGA KWENYE RAMANI YA DUNIA


Maximo kocha mpya wa Yanga amesema ataiweka Yanga kwenye ramani ya dunia....Maximo ambae alikuwa kocha wa Taifa Stars amesema hayo akiwa hapo Jangwani wakati akitoa mikakati yake ya kuifundisha Yanga...Maximo amekamata mkataba wa miaka miwili...Maximo liwaambia waandishi wa habari kwamba TP Mazembe ya DRC Congo wanafahamika sana kwasababu wanacheza sana mechi za kimataifa la hasha na Yanga itajulikana hivyo hivyo...Bofya hapa upate habari kamili kutoka Jangwani...

WORLD CUP 2014: ROUND YA MTOANO INAANZA LEO


Round ya mtoano inaanza leo...Timu 16 bora zilizobaki sasa zinaanza safari ya kuwania ubingwa wa dunia...Timu ikifungwa inafunga virago na kuelekea nyumbani kwao...Mechi ya za leo ni kati ya Brazil na Chile saa 1 usiku na badae saa 5 mechi kati ya Colombia na Uruguay...Usikose kuangalia...


EPL: LUKE SHAW AINGIA OLD TRAFFORD


Luke Shaw beki mkali kutoka Southampton na pia anaichezea timu ya taifa ya Uingereza amechukuliwa na Manchester United kwa pound za Uingereza milioni 27 kwa kuanzia...Dau litapanda kutoka milioni 27 mpaka milioni 31 pound za Uingereza kutokana na uchezaji wake...Luke Shaw mwenye umri wa miaka 18 atakuwa dogo tajiri sana...Ryan Giggs ambae ni kocha msaidizi wa Man United amesema huyu beki wa kushoto anakipaji na anauwezo wa kuwa mchezaji bora...Bofya hapa upate habari zaidi...

Friday, 27 June 2014

WIMBLEDON 2014: SERENA NA SHARAPOVA WAINGIA ROUND YA 3


Serena Williams ambae amewahi kushinda michuano hiyo mikali mara 5 ameingia round ya 3 baada yakuchapa Chanelle Cheepers (namba 94 duniani) kutoka Afrika ya Kusini 6-1 6-1...Mechi ilitumia dakika 49 tu...Pia Maria Sharapova ameingia round ya 3 baada yakumtwanga Timea Bacsinszky 6-2 6-1...Maria alisema mechi haikuwa rahisi lakini amefurahi amesonga mbele...Bofya hapa upate habari zaidi...

RIADHA: GLASGOW 2014 MICHEZO YA COMMONWEALTH HUSSAIN BOLT ATAKUWEPO


Hussain Bolt bingwa wa riadha duniani kutoka Jamaica amesema atashiriki michuano ya Commonwealth huko Glasgow...Michuano hiyo ya ridha itafanyika tarehe 23 July mpaka 3 August...Toka Bolt aumie hajakimbia kwenye mashindano mengi makubwa hivi karibuni na anaweza asikimbie kwenye mashindanio ya mita 100 na mita 200 lakini atakimbia kwenye relay...Bofya hapa usome zaidi...

Thursday, 26 June 2014

WORLD CUP 2014: BREAKING NEWS; SUAREZ AFUNGIWA MIEZI 4


Luis Suarez amefungiwa miezi 4 kwa kumg'ata mchezaji wa timu ya Italy Giorgio Chiellini....Suarez ambaye anachezea Uruguay na Liverpool amesimamishwa kwenye shughuli zote zinazohusu mpira kwa miezi 4...Pia amepigwa faini ya pound za Uingereza 65,680 na atakosa mechi 9 za Premiership ya Uingereza....Hii ni adhabu kubwa sana ambayo ni historia katika World Cup....Mara ya mwisho mtu kapewa adhabu ni 1994 baada ya Mauro Tassotti kumpiga kipepsi Luis Enrique...Bofya hapa upate habari zaidi...

WORLD CUP 2014: GHANA YATIMUA WACHEZAJI WAKE WAWILI



Ghana imetimua wachezaji wake wawili kwa utovu wa nidhamu...Wachezaji hao ni Kevin-Prince Boateng na Sully Muntari...Boateng amesimamishwa kwa lugha chafu dhidi ya kocha wao Appiah......Muntari amesimamishwa kwa kumuumiza Moses Armah mjumbe wa kamati ya timu hiyo....Woto wawili wamesimamishwa moja kwa moja kutokana vitendo vyao hivyo vya utovu wa nidhamu...Bofya hapa upate habari zaidi...

Wednesday, 25 June 2014

NBA: LEBRON JAMES AMEAMUA KUWA FREE AGENT



LeBron James wa Miami Heat ameamua kuwa free agent kuanzia July 1 na inawezekana asichezee tena Miami Heat...Kuwa free agent anauhuru wa kuichezea timu yoyote tutokana na makubaliano baina yake na hiyo timu...Habazr hizi zilitolewa na agent wa LeBron  Rich Paul ambae aliwataarifu Miami Heat kwamba mchezaji wake ameamua kuwa free agent...Kuwa free agent haiwezi kumzuia LeBron kuendelea kuichezea Miami Heat ambayo ilipoteza ubingwa kwa San Antonio Spurs...Bofya hapa upate habari zaidi...

FURSA KWA WADAU WA MAX SPORTS: CONTINERS ZA 40 FEET ZINAUZWA...CHANGAMKENI CONTAINERS NI ADIMU SANA



Fursa kwa wadau wa Max Sports kupata Continers za 40 feet...Upitikanaji wa Containers za 40 feet huwa ni mgumu sana lakini kupitia Max Sports unaweza kupata bila shida...


Pamoja na kukupa habari mbalimbali za michezo pia unaweza kufaidika na fursa nyingi tu ambazo zinaweza kukusaidia kwenye biashara zako na maisha yako kiujumla...Endelea kuingia Max Sports upate hizi fursa...


Continer za 40 feet zinapatikana hapa Dar-es-Salaam na unaweza kuletewa popote ulipo Dar-es-Salaam au unaweza kuchukua kutumia usafiri wako kwenye yadi...Kwa habari zaidi piga simu 0658 863 355 0755 454 505 / 0716 564 262 ulizia Alex...

WORLD CUP 2014: SUAREZ MATATANI TENA


Suarez anatarajiwa kushtakiwa na FIFA kutokana na kitendo chake cha kumng'ata Chiellini begani kwenye mechi iliyochezwa jana usiku kati ya Uruguay na Italy....Hii ni mara ya 3 Suarez anafanya hicho kitendo na sasa FIFA wamesikitishwa na wamemwambia Suarez na Uruguay kuja na uthibitisho ifikapo leo jumatano usiku...Suarez anatatizo hili siku nyingi na pia alifungiwa mechi nyingi Premiership wakati akiwa na Liverpool...FIFA wanauwezo wa kumfungia Suarez miaka miwili...Kwa mtazamo wa wengi Suarez ni mpuuzi au kichwa chake kibovu na anatakiwa apate matibabu ya akili na aache kucheza kabisa...Bofya hapa upate habari zaidi...

Tuesday, 24 June 2014

WORLD CUP 2014: NEYMAR AIBEBA BRAZIL




Dogo Neymar ameibeba Brazil kwa kupachika mabao mawili safi dakika ya 17 na dakika ya 34 na kuiweka Brazil kwenye nafasi ya 16 bora...Cameroon waliambulia goli moja dakika ya 26 kutok kwa Joel Matip...Wengine waliopachika magoli kutoka Brazila ni Fred dakika ya 49 na Fernandinho dakika ya 84...Sasa Brazil wanakibarua na Chile...Kazi bado ipo...

WIMBLEDON 2014: ANDY MURRAY AANZA VIZURI

  
Andy Murray ameanza vizuri safari yake yuwania tena ubingwa wa Wimbledon mwaka huu...Murray ambae ni bingwa mtetezi aliingia kwenye court akishangiliwa sana na mashabiki na wadau wa Tennis...Murray amemfunga David Goffin 6-1 6-4 7-5...Atacheza na Blaz Rola kwenye round ya 2...

Monday, 23 June 2014

WORLD CUP 2014: MSIMAMO WA GROUP G-H

Group G
#
Country
GP
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
2
1
1
0
6
2
4
4
2
2
1
1
0
4
3
1
4
3
2
0
1
1
3
4
-1
1
4
2
0
1
1
2
6
-4
1
 
Group H
#
Country
GP
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
2
2
0
0
3
1
2
6
2
2
1
0
1
5
4
1
3
3
2
0
1
1
1
2
-1
1
4
2
0
1
1
3
5
-2
1

WORLD CUP 2014 : MSIMAMO WA GROUP D-F

Group D
#
Country
GP
W
D
L
GF
GA
GD
PTS

1
2
2
0
0
4
1
3
6

2
2
1
0
1
2
2
0
3

3
2
1
0
1
3
4
-1
3

4
2
0
0
2
2
4
-2
0
 
Group E
#
Country
GP
W
D
L
GF
GA
GD
PTS

1
2
2
0
0
8
2
6
6

2
2
1
0
1
3
3
0
3

3
2
1
0
1
4
6
-2
3

4
2
0
0
2
1
5
-4
0
 
Group F
#
Country
GP
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
2
2
0
0
3
1
2
6
2
2
1
1
0
1
0
1
4
3
2
0
1
1
0
1
-1
1
4
2
0
0
2
1
3
-2
0