Thursday, 31 July 2014
EPL: SPRAY YA WORLD CUP KUTUMIKA PREMIERSHIP
Boss wa Premiership Richard Scudamore amesema baada ya kuona mafanikio ya kutumia hiyo spray na baada ya kuongea na timu na wadau wa premiership sasa hiyo spray itatumika kwenye msimu ujao...Pia amesema premiership iko tayari kubadilika kama mabadiliko yataisaidia mchezo wa soka...Bofya hapa upate habari zaidi...
CHAMPIONS LEAGUE: CELTIC YAGARAGAZWA NA LEGIA
Celtic imegaragazwa vibaya na Legia Warsaw kwenye mechi ya round ya 3 ya kufuzu kucheza Champions League...Isingekuwa kipa Fraser Forster mabao yangekuwa mengi sana...Efe Ambrose alipewa kadi nyekundu baada ya rafu mbaya...Celtic walianza kuona lango la Warsaw lakini walijichanganya na wakalamba 2 kabla ya mapumziko...Game ilimalizika kwa mabao 4-1...Bofya hapa upate habari zaidi...
Wednesday, 30 July 2014
EPL: LUKAKU MBIONI KUBAKI EVERTON
Tuesday, 29 July 2014
GLASGOW 2014: OKAGBARE ASHINDA MBIO ZA MITA 100
Blessing Okagbare kutoka Nigeria ameshinda mbio maarufu za mita 100...Okagbare alitumia muda wa sekunde 10.85...Aliwashinda wenzake kutoka Jamaica Veronica Campbell-Bown na Kerron Stewart ambao walipata Silver na Bronze wa 4 alikuwa Asha Philip kutoka Uingereza...Okagbare ambae anamiaka 25 atakimbia mita 200 na long jump pia...Mpaka sasa Nigeria wana 10 medals...
GLASGOW 2014: BINGWA WA SQUASH DUNIANI ASHINDA DHAHABU
Bingwa wa Squash duniani na namba 1 duniani kwa upande wa wanawake ameshinda mashindano ya Squash kwenye michezo ya Commonwealth huko Glasgow Scotland...
Nicol David alimchapa Laura Massaro 12-10, 11-2, 11-5...Nicol ni bingwa wa dunia kwa miezi 99 sasa na hii ni mara ya pili anashinda dhahabu kwenye michezo ya Commonwealth...Bofya hapa upate habari zaidi...
Monday, 28 July 2014
EPL: ARSENAL YASEMA OSPINA TAYARI
Arsenal FC imekamilisha usajili wa David Ospina kipa mkali sana kutoka Nice...Ospina ambae nchi yake ni Colombia atakaa Emirates miaka 4 na amechukuliwa kwa milioni 3.2 pounds...Ospina mwenye umri wa miaka 25 atakuwa karibu na kipa namba 1 wa Arsenal Sczcesny na itabidi apambane na yeye awe namba 1...Huyu ni mchezaji wa 3 kuingia Emirates mwaka huu...Arsenal nao wameamua kuchukua vifaa vya nguvu maana huwa ni wazito kutumia pesa nyingi kununua vifaa...Bofya hapa usome zaidi....
YANGA: KAMATI KUU YAVUNJWA NA KUUNDWA UPYA
Manji na Sanga (picha: michuzi blog) |
TANZANIA U-17: RC AFUNGUA MASHINDANO YA VIJANA
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Saidi Meck Sadiq amefungua mashindano ya vijana ya kikanda yanayoitwa 'Airtel Rising Stars'...Sadiki amewaasa TFF na wadau wa mpira kuchukulia kwa uzito umuhimu wa kuwafundisha vijana michezo toka wadogo...Aliwakumbusha wadau kwamba michezo ni muhimu sana katika maendeleo yao ya elimu na pia katika kutafuta ajira au kujiajiri...Bofya hapa usome zaidi...
Sunday, 27 July 2014
BOXING: ROY JONES JR. AMTWANGA FRY
Saturday, 26 July 2014
GLASGOW 2014: BOLT ATAKIMBIA 4X100M
EPL: ARSENAL KUMYAKUA BEKI CALUM CHAMBERS
Arsenal FC karibu inamchukua beki makini kutoka Southampton Calum Chambers...Chambers ambae anaichezea Uingereza kwenye timu ya vijana chini ya miaka 19 alichekiwa na madaktari Ijumaa tayari kuingia Emirates...Arsenal wametoa milioni 16 pounds kumyakua beki huyu mkali...Chambers sasa ni mchezaji wa 3 kuingia Arsenal kabla msimu haujaanza wengine ni Alexis Sanches na Mathieu Debuchy...Bofya hapa upate habari zaidi...
F1: GARI YA HAMILTON YAWAKA MOTO
Gari ya Lewis Hamilton imewaka moto katika practice ya mwisho kabla ya mashindano ya Hungary GP kesho...Nico Rosberg ataanza kwenye pole na hii sio habari njema kwa Lewis kwani anapoteza points ambazo zingemwezesha kuwa bingwa...Hii ni mara ya 6 sasa Lewis anapata matatizo kwenye qualifying na kukosa nafasi ya kwanza...Mercedes wanasema wanadhani Hamilton alipata tatizo la kuvuja kwa mafuta...Bofya hapa upate habari zaidi...
EPL: DROGBA ARUDI CHELSEA
Friday, 25 July 2014
GLASGOW 2014: TANZANIA YAANZA VIZURI KWENYE SWIMMING
Tanzania imeanza vizuri kwenye mashindano ya kuogelea...Ammaar Ghadiyali alikuwa kinara wa kuogelea baada ya kushinda mzunguko wa kwanza wa mita 50 za Butterfly...Alitumia sekunde 28.11 na kuwaacha mbali wapinzani wake kutoka St. Vincent na Granadines...Usisahau kuangalia mashindano haya yanayoendelea huko Glasgow Scotland...Bofya hapa upate habari zaidi...
GLASGOW 2014: UFUNGUZI WA MICHEZO YA COMMONWEALTH
Thursday, 24 July 2014
F1: MEXICO GP TO MAKE A COMEBACK SINCE 1992
Mexico Grand Prix back again in 2015 after a long absence.
F1 boss Bernie Ecclestone has confirmed and added it would benefit both sides.
It has been 23 years from the last race at Autodromo Hermanos Rodriguez
The track was used from 1963-1970 and 1986-1992.
The last driver to win the Mexican GP was Nigel Mansell from UK with team Williams-Renault...
Mexican Grand Prix winners | ||
---|---|---|
Year
|
Driver
|
Team
|
1992
|
Nigel Mansell (GB)
|
Williams-Renault
|
1991
|
Riccardo Patrese (Ita)
|
Williams-Renault
|
1990
|
Alain Prost (Fra)
|
Ferrari
|
1989
|
Ayrton Senna (Bra)
|
McLaren-Honda
|
1988
|
Alain Prost (Fra)
|
McLaren-Honda
|
1987
|
Nigel Mansell (GB)
|
Williams-Honda
|
1986
|
Gerhard Berger (Aust)
|
Benetton-BMW
|
Azerbaijan is a rich oil nation and they want a street race in Baku.
GLASGOW 2014: MICHEZO YA COMMONWEALTH YAANZA RASMI
Michezo ya Commonwealth imeanza rasmi huko Glasgow Scotland...Michezo hii inahusisha nchi 71 ambazo zilitawaliwa na Uingereza miaka ya nyuma...Tanzania tulijiunga na Commonwealth mwaka 1961 na mwaka 1962 tulianza kushiriki michezo ya Commonwealth..1974 ndio mara ya kwanza Tanzania inapata medani ya dhahabu ambayo Filbert Bayi ndio alioipata huko Christchurch New Zealand...
Malkia wa Uingereza alifungua michezo hii rasmi mbela ya watu 40,000 waliokuwa uwanja wa Celtic Park na mamilioni waliangalia ufunguzi huo kwenye tv..Bofya hapa upate habari zaidi...
ELP: MANCHESTER UNITED YAANZA VIZURI CHINI YA KOCHA MPYA
Ander Herrera |
Wednesday, 23 July 2014
FURSA: WADAU WA MAX SPORTS CHANGAMKIENI FURSA NYINGINE
Wadau wa Max Sports kuna fursa hapa ya kuanzisha garage na car wash kwa wale wanaopenda biashara hiyo...Hebu soma hiyo picha hapo juu na upate maelezo ya vitu ambavyo ni vipya kabisa na vinapatikana hapa Dar es salaam...Piga simu iliyo hapo juu kwa maelezo zaidi...
Tuesday, 22 July 2014
BRAZIL: DUNGA KOCHA TENA
Carlos Dunga amechaguliwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Brazil...Hii ni mara ya 2 Dunga anaifundisha timu ya Brazil mara ya kwanza ilikuwa 2006 mpaka 2011...Dunga pia aliwahi kuichezea timu ya ushindi ya Brazil mwaka 1994 wakati akiwa captain...Dunga anachukua nafasi ya Luiz Filipe Scolari ambae aliamua kustaafu baada ya kukosa kombe la dunia...Bofya hapa upate habari zaidi...
LA LIGA: REAL MADRID YAMNYAKUA MSHINDI WA GOLDEN BOOT
Real Madrid imechukua kifaa cha ukweli na mshindi wa Golden Boot kwenye World Cup iliyopita James Rodriguez...Forward huyu mwenye miaka 23 kutoka Colombia amechukuliwa kwa pound milioni 63...Hii transfer sasa ni ya 4 kwa pesa nyingi iliyotumika kumyakua mchezaji...Transfer ya bei mbaya ni ile ya Gareth Bale na kufuatiwa na Cristiano Ronaldo na Luis Suarez...Bofya hapa upate habari zaidi...
EPL: PATRICE EVRA AHAMIA JUVENTUS
Partice Evra amekamilish uhamisho wake kutoka Man U kwenda Juventus...Evra amechukuliwa wa pound milioni 1.2...Evra aliingia Man u kutokea Monako kwa pound milioni 5.5 miaka 8 iliyopita na ameshinda Premiership mara 5 akiwa na Man U...
Evra aondoka Man U akimshukuru sana Sir. Alex Ferguson kwa kumwezesha awe captain na kumkumbusha hakuna aliye juu ya club...Bofya hapa upate habari zaidi....
EPL: STEVE GERRARD ASTAAAFU SOKA LA KIMATAIFA
Steve Gerrard ameamua kustaafu soka la kimataifa baada ya kutumikia nchi yake kwa miaka 14...Gerrard ambae alianza kuitumikia nchi yake mwaka 2000 chini ya kocha makini Kevin Keegan katika ubingwa wa Ulaya...Gerrard ana 114 caps (mechi 114 za kimataifa alizoichezea nchi yake) na game yake ya mwisho ilikuwa dhidi ya Costa Rica...
Kijana Steve akiwa na Kevin Keegan akiwa |
Gerrard amecheza kwenye timu ya taifa ya Uingereza chini ya makocha 6 ambao ni Kevin Keegan, Peter Taylor, Sven Goran-Eriksson, Steve McClaren, Fabio Capello na Roy Hodgson...Katika muda huo amefunga mabao 14...Goli lake la kwanza la kimataifa lilikuwa mwaka 2001 walipoichapa Ujerumani 5-1 huko Munich...Bofya hapa upate habari zaidi...
Monday, 21 July 2014
EPL: LIVERPOOL IKO MBIONI KUMYAKUA LOIC REMY
AFCON 2015: TAIFA STARS YATOKA SARE NA MAMBAS
Mchezaji wa Stars akimtoka mtu...(Picha kutoka Shaffidauda.com) |
Taifa Stars jana jioni ilishindwa kushikilia ushindi baada ya mchezo kumalizika 2-2...Khamis Mcha ambaye alikuwa substitute ndio aliyekuwa kinara wa magoli...Nooij kocha wa Taifa Stars alisaidia kutoa siri ya Mambas jinsi gani ya kuwakabili na ikasaidia...Mambas hawajawahi kupoteza mechi dhidi ya Stars...Tusubiri marudiano huko kwao sasa...Sehemu nyingine Uganda imeshinda mechi yake dhidi ya Mauritania 2-0 huko Kampala Uganda...Bao la kwanza ililikuja kipindi cha 2 dakika ya 49 baada ya Brian Majwega kunyuka mkwaju safi...Bofya hapa upate habari zaidi...
Sunday, 20 July 2014
THE OPEN CHAMPIONSHIP: RORY MCLLROY BINGWA
Rory Mcllroy ashinda British Open leo baada ya kufukuziwa na Sergio Garcia na Rickie Fowler...Rory alishinda kwa stroke 2 na alipata 71 na ameondoka na kitita cha dola za kimarekani milioni 8...Dogo kutoka Ireland ya kaskazini ameshinda Major ya 3 sasa akiwa na miaka 25 tu...Rory sasa ni namba 2 duniani kwenye rankings za golf...Bofya hapa upate habari zaidi...
F1: HAMILTON AIBUKA MSHINDI WA 3 WAKATI ALIANZA WA 20
Hamilton alianza wa 20 kutokana na ajali mbaya aliyoipata jana baada ya gari yake kupata matatizo ya breaks...Mshindi wa 2 alikuwa Bottas na mshindi wa 4 Sebastian Vettel...Bofya hapa upate habari zaidi...
AFCON 2015: TAIFA STARS UWANJANI LEO NA MAMBAS
Taifa Stars watinga uwanjani leo kwenye uwanja wa taifa kupambana na 'Mambas' kutoka Mozambique...Hii ni mechi muhimu sana ya round ya pili katika kampeni ya kuelekea AFCON 2015...Kocha wa Taifa Stars Mart Nooij anakutana na timu yake ya zamani leo...Nooij aliwafundisha Mambas kati ya mwaka 2007 na 2011...Hii ni mara ya 5 timu hizi zinakutana kwenye michuano ya AFCON...Max Sports inawatakia heri Taifa Stars kwenye mechi yao ya leo...Bofya hapa usome zaidi....
Saturday, 19 July 2014
EPL: ROBBIE FOWLER ATEULIWA BALOZI WA LIVERPOOL
Robbie Fowler amerudi tena Liverpool kama Balozi...Striker hatari sana ambae alianzia maisha yake ya soka hapo Liverpool academy na kungia timu ya wakubwa 1993...Amecheza mechi 369 na kati ya hizo alipata mabao 183...Robbie amesema ilikuwa heshima kuichezea Liverpool na miaka 30 hapo Liverpoool imekuwa ni kipande cha maisha yake...Kwa wale wadau wa Merseyside anamuita Fowler "Legend" kwani huyu striker alikuwa mkali sana na anakasi kubwa sana...Hapo chini angalia jinsi alivyokuwa anacheza enzi zake...Hongera sana Balozi Robbie Fowler...
Friday, 18 July 2014
LA LIGA: TONI KROSS SASA NI MCHEZAJI RASMI WA REAL MADRID
Toni akiwafurahisha mashabiki wa Madrid |
Toni Kross amekamilisha usajili wake Real Madrid kutoka Bayern Munich...Kross amechukuliwa na Real Madrid kwa milioni 24 pound za Uingereza...
Toni na Ancelotti |
Mwenyekiti wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amemshukuru Kross kwa muda wake Bayern na anamtakia heri yeye na familia yake huko Madrid...Bofya hapa upate habari zaidi...
EPL: VAN GAAL ASEMA SURA MPYA ZITAKUJA
Kocha mpya wa Manchester United mesema inawezekana sura mpya zikajitokeza lakini hii ni baada ya yeyey kocha kuwaangalia wachezaji aliokuwanao kwanza...Atachukua wiki 3 au 4 kuangalia squad yake itavyojituma chini yake alafu ataamua kama aongeze wachezaji au la...Van Gaal pia amesema ataangalia jinsi ya kuwatumia vizuri Rayan Giggs, Nicky Butt, Phil Neville na Paul Scholes kwenye mambo yake ya ukocha...Angalia hapo chini press conference yake ya kwanza toka ajiunge na club hiyo...
BOXING: PAC-MAN KUZICHAPA NA CHRIS ALGIERI
Pac-Man |
Chris Algieri |
Mkanda utaokuwa unatafutwa na Chris Algieri ni wa WBO welterweight ambao umeshikiliwa na Pac-Man...Algieri alipanda ngazi baada ya kuntwanga Provodnikov hivi karibuni...Hii ni mara ya 2 Pac-Man anazichapa huko Macau...Mwaka jana alizichapa na Brandon Rios hatika huo mji unaojulikana sana duniani kwa kamali...Usikose kuangalia...
Thursday, 17 July 2014
EPL: ARSENAL YAIMARISHA KIKOSI TENA KWA KUMCHUKUA DEBUCHY
Wednesday, 16 July 2014
GLASGOW COMMONWEALTH GAMES: DR. KIKWETE AWATAKIA HERI WANARIADHA
Rais Dr. Kikwete akimkabidhi nahodha wa timu ya riadha (picha: www.ikulu,go.tz) |
Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete amewatakia heri timu ambayo itatuwakilisha kwenye michezo Commonwealth huko Glasgow...Rais Kikwete amewaambia wanariadha 39 amabo watatuwakilisha kwamba wanadeni na kulilipa hilo deni ni kurudi na ushindi...Amesema pia Tanzania kuna ukame wa medals na sasa ni wakati wa kubadilisha mambo...Rais amewashukuru Tanzania Olympic Committee pamoja Wizara ya Vijana na Wizara ya Mambo ya Nje kwa kuhakikisha timu iko katika hali ya kimataifa na iko tayari kupambana katika hiyo michezo ya Commonwealth...Bofya hapa upate habari zaidi...
EPL: ARSENAL WAKO TAYARI KUTOA MAMILIONI KUMCHUKUA KHEDIRA
Arsenal FC iko tayari kutoa milioni 20 pound za Uingereza kunyakua midfielder hatari sana kutoka Real Madrid Sami Khedira...Inasemakana Khedira atakubali mkataba wa miaka 4 na Arsenal...Arsene Wenger atakuwa ameimarisha kikosi kwa kusajili watu 2 sasa baada ya kumchukua Alexis Sanchez...Mjerumani Khedira inasemekana ameboreka na Real Madrid na amegoma kusaini mkataba mpya na timu hiyo...Bofya hapa upate habari zaidi...
Tuesday, 15 July 2014
CHESS: TANZANIA KWA MARA YA KWANZA YAPATA FIDE RANKINGS
Kwa mara ya kwanza katika historia Tanzania imepata FIDE (Shirikisho la Chess Duniani) rankings...Wachezaji 5 kutoka Tanzania wamepata ranking hizo za FIDE...Mwenyekiti wa Tanzania Chess Association, Geoffrey Mwanyika, alithibitisha haya na kuwataja waliopata rankings hizo ni pamoja na yeye Mwenyekiti (1922) Hemed Mlawa (1799) Yusuf Mdoe (1707) Mwaisumbe Emmanuel (1685) na Godlove Kimaro (1681)...
Georfrey Mwanyika (kushoto) akiwa na bingwa wa dunia Vishy Anand (katikati) |
Mwanyika amesema sasa hawa wote wananafasi ya kuwa International Master na Grand Master...Sasa Tanzania kwa mara ya kwanza iko mbioni kutafuta Grand Master wa kwanza...FIDE walitangaza hizi ranking mpya baada ya michuano iliyofanyika hivi karibuni kati ya Kenya na Tanzania iliyoandaliwa na Spicenet na Kasparov Chess Foundation...Safi sana wachezaji wote wenye hizo ranking za kimataifa na Max Sports pamoja na wadau tunawatakia heri katika kutafuta Grand Master wa kwanza wa Tanzania...
EPL: LIVERPOOL SANA YAMTAKA MARCO REUS
Liverpool FC au wazee wa Anfield wanamtaka sana dogo kutoka Borussia Dortmund Marco Reus....Reus alitoswa na Barca wakati Suarez alipochaguliwa na Barc...Liverpool wanahitaji sana striker mkali baada ya kumpoteza Suarez...Rogers yuko tayari kutoa milioni 44 pound za Uingereza amchukue Reus...Pata habari zaidi hapa....
AFRICAN YOUTH CHAMPIONSHIP: TIMU YA TAIFA YA VIJANA WAKO TAYARI KUWAKABILI AMABIMBOS
Serengeti Boys timu yetu ya taifa ya vijana (U-17) ijumaa itaingia uwanjani na vijana wenzao kutoka Afrika ya Kusini...Timu hiyo inayojulikana kama Amajimbos watachuana na Serengeti Boys kwenye mashindano ya awali wa African Youth Championship katika uwanja wa Azam Complex huko Chamanzi Dar es Salaam...Kocha mpya wa Serengeti Boys amesema wamewaweka vijana wake tayari kwa mechi ya ijumaa wakijua kwamba madogo wa Amajimbos wanacheza kwa misuli na kwamba itakuwa mechi ya kutumia nguvu zaidi...Bofya hapa usome zaidi...
WORLD CUP 2014: KIGEZO CHA MESSI KUSHINDA GOLDEN BALL
Monday, 14 July 2014
WORLD CUP 2014: LUIZ FILIPE SCOLARI ABWAGA MANYANGA
Subscribe to:
Posts (Atom)