Monday 29 February 2016

CAPITAL ONE CUP 2016: KIPA WILLY CABALLERO AIPA KOMBE MANCHESTER CITY


Kipa wa Manchester City, Willy Caballero, ameisaidia timu yake kunyakua kombe la Capital One jana usiku...Mechi ilikuwa kali sana na ya kasi pia vikumbo vilikuwa vingi...Liverpool mwishoni walifanikiwa kusawazisha bao kupitia kwa Coutinho dakika ya 83 na mpira ukaisha kwa draw...


Dakika za nyongeza Liverpool walikosa nafasi nyingi za kufunga lakini hali ilikuwa drw mpaka mwisho wa dakika za nyongeza...Matuta ndio yaliosaidia Manchester City kupumua baada ya kipa Willy Caballero kupangua shuti za Coutinho na Lalana...


Manchester City ya Pellegrini imefanikiwa kupata kombe mwaka huu...Hongera zao...Bofya hapa upate habari zaidi.

Sunday 28 February 2016

EPL:MAN U YAOKOLEWA NA DOGO RASHFORD TENA


Dogo hatari wa Man U, Marcus Rashford, amepata mabao 2 muhimu sana dhidi ya Arsenal kwani Man United wanachechemea na dogo amepata nafasi ya kuonyesha ulimwengu na yeye yumopo...Katika meshi 2 kapata mabao 4 na sasa lazima atachukua namba ya mtu tuwe tunamuona...Bofya hapa upate habari zaidi.

Saturday 27 February 2016

EPL: RATIBA YA MECHI ZA LEO (GMT)


FIFA: GIANNI INFANTINO RAIS MPYA FIFA


FIFA jana ilichagua kiongozi mpya wa Shirikisho hilo katika zoezi la kupiga kura lililofanyika Zurich...Gianni Infantino amekua Rais mpya wa FIFA... Infantino alipata kura 115 na alimpita Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa kwa kura 27...Infantino amechukua nafasi ya Sepp Blatter ambae alikuwa rais wa FIFA toka 1998 na sasa Blatter amefungiwa miaka 6 kutojihusisha na shughuli zozote za mpira...Rais mpya wa FIFA alikuwa hata hana mpango wa kuwania urais lakini Michel Platini alipoacha kuwania urais Infantino aliingia kwenye kinyan'ganyiro cha urais...Ameahidi kusafisha FIFA na kurudisha sifa ya mpira...Bofya hapa upate habari zaidi.

NIGERIA: SAMSON SIASIA RUDI TENA KUONGOZA TIMU YA TAIFA NIGERIA


Samson Siasia amechaguliwa kuiongoza timu ya taifa ya Nigeria baada ya Sunday Oliseh kuachia ngazi Ijumaa iliyopita...Oliseh aliondoka kutokana na kutoelewana na Shirikisho la Soka Nigeria kuhusu mkataba na mshahara wake...Siasia aliwahi kufundisha Super Eagles December 2010 mpaka October 2011...Bofya hapa upate habari zaidi.

Friday 26 February 2016

EGYPT: MARTIN JOL KOCHA MPYA AL AHALY


Kocha wa zamani wa Tottenham na Fulham Martin Jol amechaguliwa kuwa kocha wa timu kubwa huko Egypt ya Al Ahly...Jol amechukua kiti cha Jose Peseiro ambae ameenda Porto...Kwa sasa timu kubwa zenye upinzani mkubwa sana Al Ahly na Zamalek zina makocha wapya...Al Ahly sasa wanaongoza ligi wakifuatiwa na mabingwa wa mwaka jana Zamalek....Bofya hapa upate habari zaidi.

FIFA: WAJUMBE KUTOKA TANZANIA WAMEONDOKA KWENDA KUPIGA KURA YA KUCHAGUA KIONGOZI WA FIFA



Wajumbe kutoka Tanzania wakiongozwa na Rais wa TFF Jamal Malinzi wameondoka jana kuelekea Zurich Uswiss kushirika zoezi la kumpata Rais mpya wa FIFA...Team ya Tanzania pia yupo Katibu Mkuu Celestine Mwesingwa na Makamu Rais Wallace Karia...Mwesigwa alisema Tanzania itafuata muongozo wa CAF katika zoezi la kupiga kura na kwa sasa CAF imesema itampigia kura Salman bin Ibrahim al-Khalifa...Pamoja na hayo Mwesigwa hajui Malinzi atampigia nani kwani upigaji kura ni siri ya mpiga kura...




Mshindi atapatikana endapo atakuwa na 2/3 ya kura au kura 138 kama hamna mtu atapata hiyo watapiga kura ya 2 ambapo atakayeshinda kwa kura zozote (Simple Majority) atakuwa Rais wa FIFA...Bofya hapa upate habari zaidi.

Thursday 25 February 2016

BRAZIL: PICHA AMBAZO HAZIJAWAHI KUONEKANA MPAKA SASA ZA PELE, GARINCHA NA TIMU YA TAIFA YA BRAZIL MWAKA 1966 ZAVUTIA WENGI UINGEREZA

Pele akiwa na Captain Bellini (Picha: Neil Perkins)

Mwaka 1966 timu ya taifa ya Brazil ilisafiri kwenda kushiriki World Cup huko Uingereza...

VODACOM PREMIER LEAGUE: AZAM YASHIKWA SHATI SOKOINE MBEYA


Azam FC imerudishwa nyuma katika mbio zake za kuipita Yanga kwa kushikwa shati huko uwanja wa Sokoine Mbeya...Draw iliyopatikana huko Mbeya sio habari njema kwa mashabiki wa Azam FC kwani kasi inapungua ya kuwania kombe la ligi...Prisons waliwashika shati na mpaka kipenga cha mwisho ubao ulisoma 0-0...Azam sasa bado wana points 46 na wanahitaji ushindi haraka...Bofya hapa upate habari zaidi.

ARUSHA: VIJANA KUNOLEWA KATIKA MCHEZO WA RUGBY (RAGA)


Vijana kutoka shule 30 watafundishwa mchezo maarufu wa Rugby kuanzia tarehe 29 February...Shule 11 katika Wilaya 3 za Arusha zinanolewa kwa siku 4...Mafunzo hayo yameandaliwa na Bhubese Pride kutoka Uingereza...Shule zitazohusika na zoezi hili ni Meru, Magereza, Makumbusho, Levolosi, Ngarenaro Primary, Illboru Secondary, Ngaresh, Lashaine, na Orkeswa Primary na Sekondary...Pamoja na kufundisha vijana waalimu 16 nao watafundishwa Rugby...Bofya hapa upate habari zaidi.

F1: IFIKAPO 2017 MAGARI YA F1 YANATAKIWA KUFUNIKWA KUMLINDA DEREVA


Magari yote ya Formula One yanatakiwa kufunikwa kumlinda dereva...


Habari hii imetoka kwenye chombo kikubwa kinachoandaa mashindano ya magari ya F1, FIA, na inataka magari wabadilishwe ifikapo mwaka 2017...


Team ya Red Bull ambayo gari lake linaendeshwa na Daniel Ricciardo wamesema watatoa proposal ya kuimarisha magari zaidi na proposal yao ni kufunika kabisa eneo analokaa dereva...Bofya hapa upate habari zaidi.

NBA: STEPHEN CURRY HAS REACHED 3 POINTS RECORD AFTER 127 MATCHES


Stephen Curry who is now a famous name in the NBA has made headlines again after reaching 3 point record in 127 matches.

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: MAN CITY YACHEZA VIZURI NA KUSHINDA KIEV


Manchester City ilikuwa kamili na sio ile timu iliyofungwa majuzi kwenye FA Cup...Katika mechi ya jana Man City iliweza kuwakabili vyema kipindi cha kwanza Dynamo Kiev na kipindi cha kwanza kupata mabao 2...Mabao yalitoka kwa Segio Aguero dakika ya 15 na David da Silva dakika ya 40...Kiev waliweza kupata bao dakika ya 58 lakini Yaya Toure aliweza kuondoa kui ya mabao kwa kutingisha nvyavu dakika ya 90...



Kwa taarifa tu Sergio Aguero amefunga mabao 16 katika mechi 17 za Champions League alizocheza...Bofya hapa upate habari zaidi.

Wednesday 24 February 2016

BARCELONA: FERNANDO ALONSO ASEMA BADO YOPO YUPO


Dereva mkali wa magari ya Formula One maarufu kwa jina la F1, Fernando Alonso, ameema haendi popote...Alonso ambae yuko na timu ya McLaren amesema haondoki mpaka mkataba wake uishe mwaka 2017...Kwa wengi katika ulimwengu wa F1 Alonso ni kati ya madereva wakali sana duniani amefanikiwa kufanya mizunguko 100 katika msimu wa awali unaoendelea huko Barcelona...Bofya hapa upate habari zaidi.

NBA: NBA KUANZISHA LIGI YA VIJANA KATIKA VIWANJA VYA JAKAYA M. KIKWETE YOUTH PARK


NBA (National Basketball Association) ya Marekani inaanzisha ligi ya vijana ya basketball...Makamu wa Rais na Mkurugenzi Mkuu wa NBA Afrika, Amadou Gallo Fall, amesema ligi hiyo itahudhuriwa na mkali wa WNBA (Women National Basketball Association) Allison Feaster...Ligi itahusisha vijana wa kiume wenye umri kati ya 12 na 14...Pia shule 30 zitashiriki ambazo ni mithili ya timu 30 za NBA Marekani...


Viwanja vya JMK Park vilijengwa kwa gharama ya milioni $2 kati ya Symbion Power, Grasshoper Soccer na timu ya English Premiership Sunderland A.F.C....Bofya hapa upate habari zaidi.

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: ARSENE WENGER AWALALAMIKIA WACHEZAJI WAKE BAADA YA KICHAPO CHA BARCA


Arsene Wenger nae ametoa kali eti analaumu wachezaji wake badala ya kuwapigia makofi Barcelona kwa kuwachapa bila ubishi 2-0...Star wa Barca, Lionel Messi, aliharibu matumaini ya Arsenal ya kusonga mbele Champions League baada ya kupata mabao 2 yote ya kipindi cha 2...Wenger amesema timu yake ilicheza kiwango cha kawaida kabisa na hawakuwa na ari ya kushinda sasa sijui kama aliangalia kipindi cha 1 au ndio kujitetea tu...



Ila amekubali Barca wazuri sana na wako 95% uhakika wa kuendelea na Arsenal wanaenda Barca kucheza tu...Bofya hapa upate habari zaidi.

Monday 22 February 2016

SNOOKER: O'SULLIVAN ASHINDA WELSH OPEN KWA MARA YA 4


Ronnie O'Sullivan mkali wa snooker ameibuka tena kwa nguvu baada ya kushida frame 7 mfululizo na kumchapa namba 3 duniani Neil Robertson 9-5...


Mchezo ulikuwa wa michuano 17 ambayo Robertson alianza kwa kushinda frame 2 za mwanzo mpaka akafika 5-2...


Sasa O'Sullivan anasema anasubiria World Championship mwezi wa 4...Bofya hapa upate habari zaidi.

BUNDESLIGA: KWA MARA YA KWANZA MECHI YASIMAMISHWA KWA KOCHA KUGOMA TUTOKA UWANJANI


Mechi kati ya Bayer 04 Leverkusen na Borussia Dortmund ilisimamishwa kwa dakiak 8 na kuanza kucheza tena baada ya kocha wa Leverkusen, Roger Schmidt, kukubali kuondoka uwanjani...Kisa kilianza wakati Pierre-Emerick Aubameyang alipopachika bao la free kick dakika ya 64 na kocha wa Leverkusen kukataa bao hilo kutokana na free-kick kupigwa sehemu tofauti...


Baada ya kukataa refa amamwambia captain msaidizi wa Leverkusen, Stefan Kiessling, amwambie kocha asepe...


Kocha akagoma ndipo refa, Felix Zwayer, akaamua kusimamisha mpira nakuondoka uwanjani...Hii ni mara ya kwanza mpira unasimamishwa kwa style hii ndani ya mechi za Bundesliga...Bofya hapa upate habari zaidi.

FA CUP: CHELSEA YAICHAPA MAN CITY YENYE VIJANA 5-1


Manchester City ilikubali kipigo cha 5-1 kutokana na uamuzi wa kupumzisha wachezaji ili waweze kucheza mechi ya Champions League Jumatano dhidi ya Dinamo Kiev huko Ukraine...Man City ilikuwa na vijana 5 kwenye squad na Chelsea walikuwa kamili...Bao pekee la Man City lilitoka kwa dogo David Faupala ambae alijitahidi sana kuonyesha uwezo wake...



Chelsea sasa watasafiri kwenda kucheza na Everton kwenye robo fainali...Bofya hapa upate habari zaidi.

DAYTONA 500: DENY HAMLIN SETS NEW RECORD AT DAYTONA 500


Denny Hamlin has won a famous NASCAR race at Daytona 500 by 0.011.

Sunday 21 February 2016

VODACOM PREMIER LEAGUE: YANGA YAIZAMISHA SIMBA 2-0


Donald Ngoma na Amis Tambwe ndio walioizamisha Simba katika mechi ya ligi iliyofanyika jijini Dar es Salaam...Watani wa jadi Simba na Yanga huwa ni gumzo kubwa hapa mjini na jana Yanga waliweza kuwanyamazisha watani kwa mabao 2...Kwa sasa Yanga wako kileleni wakiwa na points 46 na Simba wamekaa nafasi ya 3 baada ya Azam FC kushinda 3-0 dhidi ya Mbeya City...Simba na Azam wako sawa kwa points lakini Azam wako mbele kwa tofauti ya mabao...Yanga walikuwa na bahati wakati mchezaji wa Simba Abdi kutolewa nje kwa kadi nyekundu kutokana na kufanya foul mara 2...Bofya hapa upate habari zaidi.

Saturday 20 February 2016

MANCHESTER UNITED: VAN GAAL AKATA TAMAA KWA KUONA WACHEZAJI WAKUBWA WAMEMCHOKA WAKIMTAKA MOURINHO


Hali sio shwari ndani ya Old Trafford kutokana na jinsi kocha van Gaal anavyoendesha mambo...Kwa habari zinazotoka Uingereza zinasema kuwa wachezaji wakubwa wamanza kumsusia na amelijua hilo na sasa muda wowote anaweza kuondoka...Naibu Mwenyekiti wa Manchester United, Ed Woodward, bado hajaamua kumtimua van Gaal lakini inawezekana akaondoka kwakuwa wanaweza kumpoteza Jose Mourinho...Wakimpata Mourinho mapema wanaweza kumaliza nafasi nzuri na ikawasaidia katika mechi za Uefa...Bofya hapa upate habari zaidi.