Monday 6 October 2014

VPL: YANGA YAILAZA JKT RUVU 2-1

Yanga wakiwa katika Poz...(Source: Shaffydauda.com)

Dar es Salaam young Africans wamefanikiwa kuwachapa maafande wa Jeshi la Kujenga Taifa 2-1 katika uwanja wetu wa Taifa jijini Dar es Salaam...Kwenye dakika ya 32 Kevin "Cotton" Yodani alitingisha nyavu ya JKT na bao hilo lilipatikana kutoka pasi safi ya Haruna Niyonzima...Bao la 2 la Yanga lilitoka kwa Niyonzima dakika ya 73 baada ya mchezaji Hassan Dilunga kufanyiwa ndivyo-sivyo na refa kutoa mpira wa adhabu...


Mashabiki wa Yanga wakiangalia game...(Source: Shaffydauda.com)
Niyonzima alipachika bao la dead ball moja kwa moja likimwacha kipa akitoa macho kama mjusi...Dakika ya 88 Jabir Aziz aliipatia JKT bao lakufutia machozi...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment