Monday 13 October 2014

F1: LEWIS HAMILTON ASHINDA SOCHI MBELE YA PUTIN


Lewis Hamilton amefanikiwa kuongoza GP mpya ya Sochi huko Urusi na kushinda mbele ya rais wa Urusi Vladimir Putin...Hamilton ambae alianza kwenye pole position aliweza kuingia kona ya kwanza vizuri lakini Rosberg alimpita kwa kasi na akashindwa kukata kona ya 2 ndipo ikabidi Rosberg aingie pit-stop kubadilisha matairi na Hamilton aliongoza mpaka mwisho...


Ilikuwa siku ya historia katika mashindano ya F1 kwa sababu 3, ya 1 ni Sochi GP ndio mara ya kwanza GP inafanyika huko, ya 2 Mercedes wameshinda Constructors Championship kwa mara ya 1, na ya 3 ni Lewis Hamilton amefikia rekodi ya Nigel Mansell ya muingereza aliyeshinda mashindano mengi mashindano 31...


Vladimir Putin alikuwepo kushuhudia mashindano hayo akiwa na boss wa F1 Bernie Ecclestone...Putin aliweza kuwasalimia maderreza walipoaliza mashindano kwenye chumba cha mapumziko na badae kumpa zawadi ya kombe Lewis Hamilton na mkurugenzi mkuu wa Mercedes upande wa technical Paddy Lowe...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment