Monday 27 October 2014

BAFANA BAFANA: CAPTAIN NA KIPA WA BAFANA SENZO MEYIWA AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI


Habari zinazoingia kutoka Afrika ya Kusini ni za masikitiko makubwa kutokana na kupoteza maisha kwa captain na kipa wa timu ya taifa ya Afrika ya Kusini Bafana Bafana Senzo Meyiwa...Senzo Meyiwa ambae pia ni kipa wa timu maafuru sana Orlando Pirates alipigwa risasi nyumbani kwa rafiki yake wa kike wakati akijaribu kupambana na majambazi waliovamia nyumba ya rafiki huyo...Ndani ya masaa 24 toka alipoichezea timu yake iliyoshinda 4-1 dhidi ya Ajax Cape Town captain alipoteza maisha yake...Polisi huko Afrika ya Kusini wamesema tukio hilo lilifanyika katika township ya Vosloorus maili 20 kutoka Jozi...Meyiwa alifariki alipofikishwa tu hospitali...Orlando Pirates wamesema wataongea na waandishi wa habari leo kuhusiana na kifo cha mchezaji wao...Max Sports na wadau wote wanaopenda mpira  tumepokea habari hizi kwa masikitiko makubwa sana...Pumzika kwa amani caaptain...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment