Thursday, 30 October 2014

BOXING: MIAKA 40 IMEPITA TOKA PAMBANO ILILILO CHANGAMSHA DUNIA LA 'THE RUMBLE IN THE JUNGLE'


The Rumble in the Jungle ilikuwa pambano la boxing la kihistoria lililofanyika nchini Zaire (DR Congo) mwaka 1974.


Pambano hilo lilikuwa kati ya George 'Big George' Foreman na Muhammad 'The Greatest' Ali na lilifanyika kwenye uwanja wa mpira wa 20th of May tarehe 30, October 1974.



Pambano lilikuwa kali sana na Ali aliweza kumtwanga Big George kwa knockout kabla ya round ya 8 haijaisha.

Ali alikuwa boxer mjanja sana na alimchosha sana Foreman kwa kutumia kamba kwa style yake ya "rope-a-dope".

Meneja wa Muhammad Ali, Gene Kilroy, alisema pambano hilo lilibuniwa na rais wa Zaire wakati huo Mobutu Sese Seko ili aweza kutangaza nchi yake na kuvutiaa utaalii.



Mobutu alitumia pesa nyingi sana na ukizingatia promota wa boxers wote Don King alikuwa hapa pesa kabisa wakati aliahidi dola milioni 5 za wakati huo.

Pambano hili lilifanyika saa 10 usiku kitu ambacho kilishangaza dunia...Wadau wengi walijua Ali atatwangwa tu hata corner ya Ali walikuwa wanajua Foreman mekuja kummaliza Ali.

Ali alikuwa anapendwa sana na watu na wadau wa boxing duniani.



Mmoja aliyempa ushauri Ali alikuwa kocha wa mabingwa Floyd Patterson na Mike Tyson, Cus D'Amato, Cus alimwambia Ali 'Uoga ni kama Moto-Unaweza kuunguza nyumba yako yote au unaweza kukupikia. Foreman ni mtemi-inabidi urushe konde la kwanza'...Bofya hapa upate habari za waliokuwepo na kushuhudia hilo pambano la karne ya 20.



No comments:

Post a Comment