Thursday 2 October 2014

CHAMPIONS LEAGUE: WELBECK AILAZA GALATASARAY


Galatasaray kiboko yao Danny Welbeck (Shabba Ranks)...Jana aliwachapa Galatasaray mabao 3 na Alexis akapachika na la kwake 1 na Shabba kurudi nyumbani na mpira wake kama ukumbusho...Mechi ya jana usiku ilikuwa ya Arsenal mwanzo mwisho kwani Arsenal walikuwa wanashambulia pande zote na Galatasaray ndio walijichanganya walivyoweka mabeki 3...


Arsene Wenger jana alitimiza miaka 18 toka aingie club ya Arsenal na akaamua kupanga kikosi cha maana chenye Sanchez, Welbeck, Ozil na Oxlade ambacho hakikumwangusha kabisa...Welbeck alichapa bao mapema dakika ya 22 na badae kidogo akapachika bao lingine zuri akitumia kiganja cha pembeni mpaka mashabiki wakakasirika na kutupa flare uwanjani na mchezo ukasimamishwa kidogo...Sanchez nae alipata bao dakika ya 41 alafu Welbeck akamalizia na bao kipindi cha pili dakika ya 52...Bofya hapa upate habari zaidi.



No comments:

Post a Comment