Sunday 24 August 2014

SOCCER TANZANIA: X-REAL MADRID YAIPIKU TANZANIA XI


Mechi ya jana ilikuwa nzuri sana ambayo ilirushwa Live mbele ya mashabiki zaidi ya 40,000 wakiongozwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Jakaya Kikwete...Alikuwemo pia Waziri wa Michezo Fenella Mukangara na Mkuu wa Mkoa Said Meck Sadik...


Tanzania 11 ilikuwa na wachezaji wale waliokuwa balaa miaka iliyopita na timu ya wachezaji wa Real Madrid wa zamani...Ruben De La Red ndio aliyeuwa kinara baada ya kufunga magoli yote 3 na mpira wake ukatiwa saini na Rais Kikwete...


Figo pia alikuwa kivutio kwani alicheza vizuri sana na kuonyesha mashabiki bado yuko fiti...Kwa upande wa Tanzania Shaaban Ramadhan alicheza vizuri sana na kushangiliwa na mashabiki lukuki...


Wachezaji wa amani wa bongo walionyesha jinsi walivyo kuwa wazuri enzi zao...Walikuwemo wakina Mecky Mexime na Athuman China...Mechi iliisha 3-1...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment