Saturday 2 August 2014

NBA: PAUL GEORGE WA INDIANA PACERS AUMIA VIBAYA SANA


Paul George wa Indiana Pacers aliumia vibaya sana baada ya kuvunja mifupa miliwi ya mguu wa kulia chini ya goti...Paul George ambaye pia yuko timu ya taifa ya basketball ya Marekani aliumia akiwa anacheza game ambayo timu ya tifa ilikuwa inaonyesha mashabiki jinsi walivyojiandaa huko Las Vegas Marekani...George aligonga chuma cha kushikia goal wakati akitaka kumzuia James Harden mwanzoni mwa kipindi cha 4...Inaonekana chuma hicho kilikuwa mbele karibu na court zaidi ya standard za NBA...


X-ray ya Paul George inavyoonyesha jinsi alivyo umia vibaya (twitter:NBA Central)
George alikimbizwa hospitali na kufanyiwa operation na atakaa huko siku 3 zaidi...Game ilisimamishwa na haikuendelea tena...Inavyosemekana George anaweza asicheze msimu ujao lakini bado madaktari hawajasema kama ataweza kucheza au la...Ni pigo kubwa kwa timu ya taifa ya Marekani na timu ya Indiana Pacers...Bofya hapa upate habari zaidi...



No comments:

Post a Comment