Tuesday 26 August 2014

EPL: LIVERPOOL CHALI ETIHAD STADIUM


Liverpool jana ilikumbushwa kwamba soka lazima usifanye makosa nyuma...Kosa la Alberto Moreno nyuma lilisababisha bao la kwanza kutoka kwa Stevan Jovetic...Kipindi cha kwanza kama dakika 40 hivi Liverpool walicheza vizuri na kufika golini kwa Man City mara kwa mara lakini hawakuweza kutengeneza bao...Baada ya kuchapwa dakika ya 41 Man City waliwapeleka shule Liverpool wakati Mario Balotelli akiangalia timu yake ya zamani ikiwashughulikia timu yake mpya...


Dakika ya 55 huyo huyo Jovetic aliandika bao la 2...Sergio Aguero aliingia kipindi cha 2 na baada ya sekunde 23 alitingisha wavu...Dakika ya 83 Liverpool wakazawadiwa goli la bure na Pablo Zabaleta...Man City ni kazi kama kawa ila Liverpool inabidi wajipange nyuma na wamtumie Balotelli vizuri...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment