Thursday, 7 August 2014

BOXING HISTORY: CASSIUS CLAY vs. SONNY LISTON, MIAMI BEACH 1964.

(Source: life.com)
Katika mechi ambayo iliwika na yenye ushabiki mkubwa miaka ya 60 ni kati ya Cassius Clay (Muhammad Ali) na Sonny Liston...Clay alikuwa bado mdogo na aliwika alivyopata dhahabu kwenye Olympics lakini Liston alikuwa mtoto wa kitaa na bandidu...Liston alikuwa anajulikana kwa kukaba watu mitaani na kuingia jela na kutoka mara kwa mara na hii ilifanya watu waone kwamba Clay anajitakia makubwa kwani ngumi ya Liston ilikuwa kama zege...Balaa...Wengi walikuwa wanamkimbia hawataki kupigana nae...

(source: life.com)
Kabla ya kuzichapa na Clay huko Miami mwaka 1964 tarehe 25 Frebruary Liston alikuwa bingwa wa dunia...Awali Liston alimtwanga bingwa wa zamani Floyd Patterson round ya 1 mwaka 1962 na walikutana tena baada ya miezi 10 na kumtwanga tena round ya 1 Floyd Patterson...Pia Liston alikuwa chini ya Mafia mmoja alijulikana kwa jina la Frankie Carbo ambae alikuwa kiongozi kwenye familia ya kimafia ya Lucchese...Carbo alikuwa anamiliki contract ya Liston...Clay alikuwa dogo mwenye miaka 22 anayeongea sana na kipindi hicho alikuwa anajulikana kama "The Louisville Lip" machachari sana...Hebu cheki hiyo clip hapo chini uone jinsi gani Cassius Clay alivyofanya mambo siku hiyo...


No comments:

Post a Comment