Thursday 7 August 2014

EPL: HOWARD WEBB ASTAAFU


Howard Webb refa mashuhuri sana ameamua kustafu baada ya kuchaguliwa kuwa mkurugenzi katika chama cha marefa...Webb amekuwa refa kwa miaka 25 sasa...Ameongoza mechi 500 ambazo ni za ligi ya kawaida na premiership...Webb mwenye umri wa miaka 43 alianza urefa 1989 na alianzia kwenye ligi ndogo za counties mpaka 2003 marefa wachache  walipochaguliwa kupanda daraja...Webb alikuwa refa makini lakini kuna wakati alikuwa anawapendelea sana Manchester United mpaka akawa anataniwa sana na mashabiki wa Uingereza na duniani kote...Lakini pamoja na hayo aliweza kuchaguliwa kuwa refa katika mechi muhimu ya fainali ya kombe la dunia 2010...Bofya hapa upate habari zaidi...

No comments:

Post a Comment