Sunday 31 August 2014

EPL: CHELSEA YANG'OA KISIKI KIGUMU


Kama ulikosa game ya jana itabidi uangalie magoli hapo chini maana ilikuwa game kali sana kati ya timu 2 kali...Chelsea iliweza kuifunga Everton 6-3 katika mchezo ambao ulishangaza mashabiki hata watangazaji walishangaa jinsi mabao yalivyokuwa yanafungwa...


Chelsea walianza kufunga magoli mapema sana na ilitumika sekunde 35 tu wakati Cesc Fabregas alipompasia Diego Costa na kutingisha nyavu...Dakika ya 3 Ivanovic nae alipachika bao ambalo kwa utaalam wa soka ilikuwa offside lakini macho ya linesmen hayakuona vizuri...


Everton walipambana na kucheza vizuri sana lakini Chelsea walikuwa makini kulinda lango mpaka dakika ya 45 Mirallas alipofanikiwa kupata bao...Eto'o nae aliingia kama sub kwa mara ya kwanza toka ahamie Everton na mara ya kwanza kugusa mpira bao likapatikana...Katika historia ya premiership hii mechi ni ya 7 kwa magoli mengi kufungwa...Bofya hapa upate habari zaidi.


No comments:

Post a Comment