Wednesday 3 September 2014

HISTORY: WADAU WA SIMBA MNAMKUMBUKA CUTHBERT PEMBA?


Kwa wale wadau wa Simba na Yanga wa zamani zile lazima wanamkumbuka Kaimu Katibu Mkuu wa Simba Sports Club Marehemu Mzee Cuthbert Pemba...Hapo juu utaona ni toleo la gazeti la Uhuru, Jumatatu, Decemba 19 1977...Kwenye picha kulia ni Mzee Pemba akisalimiana na Marehemu Ezekiel Grayson a.k.a Jujuman ambae alihamia Simba akitokea Yanga...Ni kama kipindi cha sasa timu zote zinavyo mgombania Okwi...Kipindi hicho pia kulikuwa na ushindani mkubwa na Yanga ilitoka kuchapwa 6-0...Kipande hichi cha historia ya soka nchini kimetolewa kwa hisani ya Elliud Pemba mdau wa Max Sports...Shukran mdau...

No comments:

Post a Comment