Sunday 14 September 2014

EPL: ARSENAL YAGAWANA POINTS NA CITY


Arsenal FC jana ilibidi igawane points na Manchester City katika game kali sana iliyofanyika mapema jana...Mechi iliisha 2-2 na Danny Welbeck aliingia kwa mara ya kwanza na kusababisha mtafaruku kwenye goli la City baada ya kuwatoka mabeki na kupiga mpira juu ya kipa na kugonga mwamba...Katika dakika 30 za mwanzo Arsenal walicheza vizuri sana na kushambulia sana lango la City...


City walionekana vizuri baada ya Yaya Toure kutokuwepo uwanjani lakini walikuwa wanajua defence ya Arsenal mbovu na wakawa wanavizia counter attacks....Aguero aliweza kutingisha nyavu baada ya mabeki kutokuwa makini dakika ya 28...


Wilshere alisawazisha kipindi cha 2 kwenye dakika ya 63 na Sanchez akawaweka Arsenal dakika ya 74...Ilikuwa game ya Arsenal lakini walinyimwa point 3 baada ya mabeki tena kuzembea na kumwachia Demichellis afunge bao dakika ya 83...Nsri ilikuwa apachike bao lakini lilikataliwa kwakuwa alikuwa off-side...Bofya hapa upate habari zaidi.


No comments:

Post a Comment