Monday 24 November 2014

F1: LEWIS HAMILTON BINGWA WA DUNIA


Lewis Hamilton amenyakua ubingwa wa mashindano ya magari ya Formula One au kwa kifupi F1 huko Abu Dhabi akiwa na team Mercedes...Hii ni mara ya 2 sasa Hamilton anachukua ubingwa wa dunia wa F1 mara ya 1 alichukua ubingwa mwaka 2008 akiwa na team McLaren...


Huko Abi Dhabi Hamilton alianza vizuri kona ya kwanza na toka hapo hakupunguza mwendo mpaka aliposhinda na pia dereva mwenzake Nico Rosberg aliyekuwa anamfukuzia alipata matatizo na gari yake...


Hamilton alisema ushindi huu ni ushindi muhimu sana katika maisha yake...Prince Harry wa Uingereza alikuwepo kushuhudia Lewis akinyakua ubingwa pamoja na baba mzazi na mchumba wa Hamilton Nicole Sherzinger...


Hongera sana Hamilton kwa kuwa bingwa wa dunia mwaka huu kutoka kwa Max Sports na wadau...Bofya hapa upate habari zaidi.


No comments:

Post a Comment