Saturday 1 November 2014

BAFANA BAFANA: MAELFU YA WATU WAJITOKEZA KUMUAGA KWA UCHUNGU CAPTAIN SENZO MEYIWA

Rais Zuma akiwa na Senzo Meyiwa enzi za uhai wake...
Mashabiki na wapenzi wa mpira wamejitokeza kwa maelfu na maelfu kumuaga Captain wa Bafana Bafana Senzo Meyiwa...Meyiwa alifariki kwa kupigwa risasi akiwa nyumbani kwa mpenzi wake wakati akijaribu kuzuia majambazi...


Watu wengi walijipanga barabarani na uwanja wa mpira wa Moses Madhiba ambao uko jijini Durban ulijaa sana wakimuaga Senzo Meyiwa kwa uchungu na majonzi makubwa sana...Kati wa waomblezaji walikuwepo rais wa shirikisho la mpira Afrika ya Kusini Danny Jordaan na wachezaji wenzake wa Orlando Pirates...


Audi Q7 nyeupe iliyobeba mwili wa marehemu Senzo Meyiwa iliingia uwanjani huku watu wote wakisimama kwa majonzi likifuatiwa na polisi na bendi ya polisi, kiongozi wa KwaZulu Natal, Edward Senzo Mchunu, rais wa shirikisho la soka, Dani Joordan, wachezaji wa Orlando Pirates na wengine wengi...


Mwili wake ulizungushwa uwanjani mara 1 na jeneza lilikuwa limefunikwa na bendera ya Afrika Kusini...Bofya hapa upate habari zaidi.


No comments:

Post a Comment