Wednesday 26 November 2014

CHAMPIONS LEAGUE: CHELSEA YAIRARUA SHALKE


Roberto Di Matteo hatasahau usiku wa jana kwani Chelsea waliigaragaza timu yake ya FC Shalke 04 kwanza kwa kufunga goli ndani ya sekunde 86 tu na pili kwa kuwapachika mabao 5-0...


Goli la John Terry la kichwa la sekunde 86 lilikuwa goli la 'chap chap' kuliko magoli yote kwa Chelsea katika Champions League na baada ya hapo Willian alipachika bao dakika ya 29...Shalke walijifungaa dakika ya 44 na Chelsea wakaingia mapumziko na mabao 3...


Drogba alifanya kazi ya ziada na dakika ya 79 alipata bao na dadae alimsaidia Ramires kupachika la 5...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment