Friday 7 November 2014

BBALL KITAA: CBE & UDSM WAPAMBANA LEO! USIKOSE!


Mechi kali ya basketball hapa mjini inasubiriwa kwa hamu kubwa kati ya College of Business Education (CBE) na University of Dar es Salaam (UDSM) leo usiku katika vwanja vya Ghymkhana....Timu zote mbili ziko tayari kupambana na UDSM wako tayari kucheza vizuri baada ya kushindwa katika game yao ya 1...Game ya eo ni kati ya game nyingi za kusherekea mwaka 1 wa BBall Kitaa...


Mratibu wa BBall Kitaa, Lawrence Karabani, amesema wanajivunia kwamba BBall Kitaa imefanikiwa sana hasa kuwaunganisha vijana wengi kuwapa shughuli ya kufanya na hasa vyuo vimehusika sana...Pia wadhanini wa BBall Kitaa Coca-Cola kupiti kinywaji cha Sprite wamefurahi sana kupewa nafasi ya kupromote basketball nchini Tanzania na kuchangamsha maisha ya vijana wengi na wataendelea kufanya kazi na wadau wa basketball Tanzania ili kuendeleza mchezo huu na kukuza vipaji...Usikose kuangalia jii game leo usiku katika viwanja vya Gymkhana...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment