Saturday, 30 April 2016

LA LAKERS: LUKE WALTON KOCHA MPYA LAKERS


Luke Walton na uongozi wa Lakers wameafikiana mkataba wa miaka kadhaa Walton awe kocha wa Lakers...Walton amemaliza mkataba wake na Golden State Warriors ambapo alikuwa kocha msaidizi na sasa kapata nafasi kwenye timu maarufu sana ya basketball nchini Marekani..Mwaka 2008 Walton alichezea timu hiyo ya Lakers...Walton atakuwa kocha wa 26 kuifundisha Lakers...Bofya hapa upate habari zaidi.

Friday, 29 April 2016

EPL: RATIBA YA MECHI ZA WEEKEND (GMT)

Saturday 30 April


15:00  Everton v. Bournemouth
15:00  Newcastle v. Crystal Palace
15:00  Stoke v. Sunderland
15:00  Watford v. Aston Villa
15:00  West Brom v. West Ham
17:30  Arsenal v. Norwich


Sunday 1 May


12:00  Swansea v. Liverpool
14:05  Man Utd v. Leicester
16:30  Southampton v. Man City

REGIONAL U-20 ATHLETICS CHAMPIONSHIP: VIJANA KUCHUANA UWANJA WA TAIFA KUANZIA LEO


Mashindano ya riadha ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 yameanza leo Uwanja wa Taifa...Mashindano haya ni yakikanda na ni muhimu sana kwani wanariadha wanaweza kufuzu kwenda kwenye mashindano ya kimataifa ya IAAF Junior Championship Bydgoszcz nchini Poland kuanzia July 19 mpaka July 24...Nchi ambazo zitashiriki ni Djibouti, Rwanda, Eritrea, Kenya, Somalia, Sudan ya Kusini, Uganda, Sudan na Zanzibar...Bofya hapa upate habari zaidi.

EPL: MSIMAMO WA LIGI MPAKA SASA

Team  PGD
1Leicester City353076
2Tottenham Hotspur353969
3Manchester City353264
4Arsenal352464
5Manchester United341259
6West Ham United341456
7Liverpool341355
8Southampton351254
9Chelsea34747
10Stoke City35-1447
11Everton34541
12Watford34-741
13West Bromwich Albion35-1141
14Bournemouth35-1941
15Swansea City35-1540
16Crystal Palace35-939
17Sunderland34-1831
18Norwich City34-2531
19Newcastle United35-2630
20Aston Villa35-4416

MLB: MKALI WA BASEBALL WA TIMU YA MARLINS, DEE GORDON, AFUNGIWA MECHI 80


Dee Gordon ambae ni baseman wa timu ya Miami Marlins na pia ni bingwa wa batting amefungiwa mechi 80 kutokana na kupatikana na madawa ya kuongeza nguvu mwilini...Major League Baseball wamesema amesimamishwa kutokana na sheria za mchezo huo wa baseball na hatolipwa...Gordon amekuwa  All-Star mara 2 na anaongoza kwa batting...Commissioner of Baseball amesema Gordon amekutwa na "exogenous Testosterone na Clostebal"...Habari ilitoka baada ya Marlins kuwachapa Dodgers na kushinda series 5-3...Bofya hapa upate habari zaidi  

Thursday, 28 April 2016

TAIFA STARS: STARS YAPATA MECHI MUHIMU YA KIRAFIKI


Taifa Stars imepata mechi muhimu sana katika calender ya mpira mwaka huu...Mechi hiyo ya kirafiki itafanyika Nyayo Stadium dhidi ya Harambe Stars tarehe 29 May...Baada ya mechi za premiership wachezaji wataingia kambini chini ya usimamizi wa kocha Charles Boniface Mkwasa...Mechi hiyo ya kirafiki pia ni njia ya kujifua wakijiweka tayari kwa mechi za kimataifa za kuwania kombe la AFCON 2017...Stars watakuwa wanasubiri kuwakabili Egypt na Nigeria ili waweze kusonga mbele...Bofya hapa upate habari zaidi.

VODACOM PREMIER LEAGUE 2016: KOCHA WA MBEYA CITY ATANGAZA KIKOSI KABLA YA MECHI DHIDI YAMTIBWA


Kocha mkuu wa Mbeya City Kinnah Phiri anayetokea Malawi ametangaza kikosi ambacho kitaenda kuikabili Mtibwa Sugar huko Morogoro...Mpira utapigwa ndani ya Manungu Stadium Jumamosi...Phiri amesema hana hofu na nafasi ambayo wako sasa lakini anauhakika wa kupata points kwenye mechi zilizobakia...Bofya hapa upate habari squad ya Mbeya City.

EUROPA LEAGUE 2016: RATIBA YA MECHI ZA LEO

THURSDAY 28TH APRIL 2016

CHAMPIONS LEAGUE 2016: BAO KALI SANA LA NIGUEZ LAIPA ATLETICO NAFASI NZURI KIDOGO


Saul Nigues, Spain U-21 International, aliwapiga chenga mabeki wa Bayern Munich kama wamesimama vile na kupachika bao safi kabisa...Bao la Niguez limewapa Atletico Madrid nafasi nzuri japo kidogo ya kuingia ungwe ya 2 wakisafi kwenda uwanja wa Bayern...Bayern walianza ovyo lakini badae walicheza mpira wa ukweli na wa akili lakini mabeki wa Atletico walikuwa wamejipanga...Torres nae hakuwa mbali na gli alipiga shuti likagonga mwamba...


Timu hizi zitakutana tena ndani ya Allianz Arena uwanja wa Bayern Jumanne ijayo...Bofya hapa upate habari zaidi.

Wednesday, 27 April 2016

DELE ALLI: DOGO WA TOTTENHAM DELE ALLI APATIKANA NA HATIA YA KUMPIGA MCHEZAJI UWANJANI


Football Association (FA) wamesema midfielder wa Tottenham Dele Alli amepatikana na hatia ya kumpiga ngumi mchezaji wa West Brom na hata refa hakuona tukio.

CHAMPIONS LEAGUE 2016: JOE HART AMEHAKIKISHA MAN CITY HAWAFUNGWI UNGWE YA KWANZA


Joe Hart amepangua mipira mawili mwishoni wakati Real Madrid wanashambulia sana mwishoni...Umakini wa Hart umeisaidia Manchester City kwenda ungwe ya 2 bila kifungwa...Real Madrid hawakuwa wenyewe nadhani pia ni kutokana na Cristiano Ronaldo kuwa nje kutokana na kuumia paja...Aguero sasa ameenda dakika 432 bila kupiga shuti linaloelekea kwenye goli na Kevin De Bruyne apipiga 62.3% ya pasi zake na ni kiwango cha chini kabisa kwa mchezaji anayecheza nafasi yake.... Hii ni dalili Manchester City wameanza kuchoka au wanapoteza mwelekeo...Bofya hapa upate habari zaidi.

Tuesday, 26 April 2016

HILLSBOROUGH INQUESTS: UCHUNGUZI WA BAINI WATU WALIOFARIKI SIKU HIYO WALIUWAWA


Mwaka 1989 kwenye nusu fainali ya FA Cup mashabiki 96 wa Liverpool walipoteza maisha uwanja wa Hillsborough...Toka siku hiyo ya huzuni kubwa sana kwa timu na mashabiki wa mpira duniani uchunguzi ulifanyika na mpaka sasa report ya iquest imetoka ikibaini mashabiki waliuwawa...Mashabiki waliuwawa kutokana na uzembe wa polisi lakini hasa uzembe wa mtu mmoja anayoitwa David Duckenfield ambaye hakujali mashabiki na usalama wao...



Pamoja na hayo mengine yaliyosababisha mashabiki kufariki ni uwanja wa Hilsborough ulikuwa unamatatizo ya usalama, Milango ambayo ilitakiwa kuwa wazi haikufunguliwa kwa wakati, Polisi na watu wa huduma ya kwanza walichelewa kutangaza hali ya hatari na mambo mengi zaidi...


Familia za wafiwa zilikuwa nje ya Mahakama ambako matokeo hayo ya uchunguzi yaliposomwa na kusema kuwa sasa haki imefuata mkondo baada ya kuzungushwa miaka yote...Walilia na wengine kuonyesha picha za ndugu zao waliofariki kutokana na mkasa huo...Bofya hapa upate habari zaidi.

Monday, 25 April 2016

BOXING: ANTHONY JOSHUA KUTETEA MKADA WAKE JUNE 25 NDANI YA O2 ARENA


Bingwa wa dunia katika uzito wa Heavyweight kupitia IBF, Anthony Jochua, atatetea mkanda wake dhidi ya mmarekani Dominic Breazeale....Dominic hajawahi kutwangwa toka awe pro boxer na kati ya ushindi wa ndondi 17 ametoa knockout 15...


Breazeale mrefu kwa inch 1 ni namba 13 duniani katika list ya wakali wa IBF chini ya Derek Chisora na David Haye...Bofya hapa upate habair zaidi.

BARCELONA OPEN 2016: RAFA NADAL AFIKIA REKODI YA OPEN CLAY COURT


Rafael Nadal au kwa jina maarufu 'King of Clay' amefanikiwa kufikia rekodi ya mashindano ya clay court ya wazi ya ushindi wa mashindano 49...Rafa amemfikia Guillermo Vilas alipofanikiwa kushinda Barcelona Open katika fainali dhidi ya Kei nishikori 6-4 7-5...Vila anayetokea Argentina alifanikiwa kufikia hiyo rekodi kati ya miaka ya 1970 na 1980...Rafa anaweza kuipita hiyo rekodi kwani ana mashindano Madrid na Rome...Bofya hapa upate habari zidi.

EPL: MSIMAMO WA LIGI MPAKA SASA

1Leicester353076
2Tottenham343968
3Man City353264
4Arsenal352464
5Man Utd341259
6West Ham341456
7Liverpool341355
8Southampton351254
9Chelsea34747
10Stoke35-1447
11Everton34541
12Watford34-741
13Bournemouth35-1941
14West Brom34-1140
15Swansea35-1540
16Crystal Palace35-939
17Sunderland34-1831
18Norwich34-2531
19Newcastle35-2630
20Aston Villa35-4416