Wednesday 6 April 2016

PANAMA PAPERS: BOSS WA FIFA GIANNI INFANTINO ATAJWA KWENYE DOCUMENTS ZA KAMPUNI ILIYOSAIDIA WATU MASHUHURI KUFICHA PESA


Gianni Infantino, Boss mpya wa FIFA, ametajwa kwenye documents ambazo zinaonyesha jinsi watu mashuhuri duniani wakiwemo maraisi na mawaziri wanavyoficha pesa kukwepa kodi...Hizo documents zinajulikana kama 'Panama Papers' na zimetoka kwenye kampuni ya binafsi ya sheria nchini Panama...




Kampuni hiyo jina lakie ni Mossack Fonseca na hizo documents ziliibiwa kupitia mitandao na sasa zimeibua mtazamo mpya kuwa kumbe watu wengi wanakwepa kodi duniani...Kwa upande wa Infantino ni kwamba hizo documents zinazungumzia watu ambao aliwahi kufanya nao mkataba zamani na hao watu wameshahusishwa na rushwa....


Hugo Jinkis, anahusishwa na dili la Uefa na rushwa

Watu hao wanaitwa Hugo Jinkis na Mariano Jinkis ambao walinunua TV rights za Uefa Champions League na baada ya muda mfupi tu wakauza hizo TV rights mara 3 na kuondoka na pesa nyingi sana...Kipindi hicho mkataba huo ulipitishwa na Gianni Infantino ambae alikuwa Mkurugenzi wa Uefa...


Mariano Jinkis akiwa amekamatwa na polisi pamoja na
mzee wake Hugo Jinkis

Infantino amesikitika watu kumfikiria vibaya na FIFA imesema hiyo tender alishinda mwenye dau kubwa na ilikuwa halali...Bofya hapa upate habari zaidi.


No comments:

Post a Comment