Friday 15 April 2016

EUROPA LEAGUE 2016: LIVERPOOL YAIDUWAZA DORTMUND NA MASHABIKI WAKE


The Kop jana usiku paliwaka moto kwani Liverpool ilikuwa imeshajulikana inatolewa nje ya michuano ya Europa au 'Uefa ndogo' kwa msemo wa kitaa lakini la hasha...Kama umewahi kusikia timu inaitwa 'The Comeback Kings' basi jana hiko jina lilijulikana kama la Liverpool moja kwa moja...Mechi yao dhidi ya Dortmund haikuwa rahisi kabisa kwani Dortmund wamesimama na ndio walionza kufunga mabao...Liverpool mara 2 kwenye mechi hiyo walihitaji mabao matatu kufuzu...


Hali ilikuwa tete sana tena siku ambayo Liverpool walikuwa wanakumbuka miaka 27 iliyopita mashabiki 96 walipoteza maisha yao katika siku ya 'Hillsborough disaster'...Kabla mpira kuanza walitoa heshima kwa waliopoteza maisha kwa kukaa kimya kwa dakika 1...Dortmund walikuwa mbele mapema dakika ya 5 kupitia bao la Henrikh Mkhitaryan na muda mfupi badae Pierre-Emerick Aubameyang akapachika bao dakika ya 9...Mashabiki wakajua leo ndio bye bye lakini ngoma ikaendelea kuchezwa na Divock Origi aliwapa matumaini alipofunga baodakika ya 48...



Liverpool walianza kwa kushambuliwa sana na Dortmund ila badae waliweza kutulia na kucheza mpira wa maana...Reus wa Dortmund kwenye dakika ya 57 akapachika bao na kurudisha matumaini ya Liverpool nyuma....Dakika ya 60 Philippe Coutinho alifanikiwa kurudisha matumaini japi finyu lakini alibadelisha game...Dakika 10 baadda ya bao hilo Mamadou Sakho akapachika bao na sasa angalau matumaini yakarudi ingawa dakika zilikuwa zinayoyoma...


Dakika za lala salama umati wa the Kop uliruka juu kwa kushangilia sana baada ya bao la Dejan Lovren kutikisa nyavu....Kweli Liverpool imeshangaza hadi mashabiki kwa kuwa timu ambayo hata ikichapwa hurudisha mabao na kushinda...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment