Sunday 10 April 2016

BOXING: ANTHONY JOSHUA AMTANDIKA CHARLES MARTIN ROUND YA 2 NA KUNYAKUA UBINGWA WA IBF


Anthony Joshua kutoka England amekuwa bingwa wa heavyweight wa mkanda wa IBF baada ya kumchapa Marekani Charles Martin...Martin alikula jabs na makonde yakutosha hasa ya kulia na refa kusitiaha pambano round ya 2 baada ya kuona anaumia...


Joshua ni bingwa wa ndondi za Olympics na sasa kwa mara ya kwanza anakuwa bingwa wa heavyweight...


Joshua ni kati ya watu 3 duniani ambao baada ya kuwa bingwa wa Olympics anakuwa bingwa wa heavyweight...Wengine ni Muhammad Ali na Leon Spinks...Mwaka 1960 Ali alikuwa bingwa wa Olympics na mwaka 1964 akamtandika Sonny Liston na kuwa bingwa wa heavyweight...


Mwaka 1976 Leon Spinks Alipata dhahabu ya Olympics na badae mwaka 1978 alimchapa Ali...Huko mbeleni sasa inaonekana kama Joshua atakutana na bingwa mwingine wa Uingereza Tyson Fury...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment