Monday 4 April 2016

MANCHESTER UNITED: SIR BOBBY CHARTON APEWA HESHIMA KUBWA KWA KUPEWA ENEO LENYE JINA LAKE OLD TRAFFORD


Sir. Bobby Charlton ni living legend wa Manchester United na kutaokana na heshima yake sehemu ya kusini wa Old Trafford umepewa jina lake...


Jana kabla ya kuanza game ya Manchester United dhidi ya Everton eneo hilo lilizinduliwa mbele ya mashabiki wengi na pia mbele ya wasio mashabiki lakini wanamkubali Sir Bobby kutokana na mchango wake Manchester United...


Sir. Bobby ambae sasa ni mmoja wa wakurugenzi wa club aliingia Manchester mwaka 1953 na kucheza mechi 758 na kufunga mabao 249...Alichezea timu ya England iliyoshinda World Cup ya mwaka 1966...


Sir Bobby alikuja uwanjani na mke wake Norma na Makamu Mwenyekiti wa club ya Manchester Ed Woodword...Eneo la kusini la uwanja ni eneo ambalo halijabadilishwa toka uwanja ujengwe mwaka 1910 na ndio sehemu wakurugenzi wanakaa au kwa jina maarufu 'directors box'...


Alinusurika kifo mwaka 1958 baada ya ndege iliyobeba wachezaji wa Manchester United kuanguka huko Munich na kuua watu 8...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment