Tuesday 26 April 2016

HILLSBOROUGH INQUESTS: UCHUNGUZI WA BAINI WATU WALIOFARIKI SIKU HIYO WALIUWAWA


Mwaka 1989 kwenye nusu fainali ya FA Cup mashabiki 96 wa Liverpool walipoteza maisha uwanja wa Hillsborough...Toka siku hiyo ya huzuni kubwa sana kwa timu na mashabiki wa mpira duniani uchunguzi ulifanyika na mpaka sasa report ya iquest imetoka ikibaini mashabiki waliuwawa...Mashabiki waliuwawa kutokana na uzembe wa polisi lakini hasa uzembe wa mtu mmoja anayoitwa David Duckenfield ambaye hakujali mashabiki na usalama wao...



Pamoja na hayo mengine yaliyosababisha mashabiki kufariki ni uwanja wa Hilsborough ulikuwa unamatatizo ya usalama, Milango ambayo ilitakiwa kuwa wazi haikufunguliwa kwa wakati, Polisi na watu wa huduma ya kwanza walichelewa kutangaza hali ya hatari na mambo mengi zaidi...


Familia za wafiwa zilikuwa nje ya Mahakama ambako matokeo hayo ya uchunguzi yaliposomwa na kusema kuwa sasa haki imefuata mkondo baada ya kuzungushwa miaka yote...Walilia na wengine kuonyesha picha za ndugu zao waliofariki kutokana na mkasa huo...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment