Thursday 14 April 2016

KOBE BRYANT: KOBE BRYANT AGONGA POINTS 60 SIKU YAKE YA MWISHO


Kobe Bryant anajulikana kwa majina mengine maarufu sana 'The Black Mamba' au 'KB24' au 'Vino' alefanikiwa kuingiza points 60 katika game yake ya mwisho kabisa...


Kobe ameshangaza umati wa watu kwani amejishangaa mwenyewe kupata points 60 na hapo awali Shaquille O'Neal alimwambia anataka kuona points 50 na Kobe akagonga na 60.



Mechi yake ya mwisho ilikuwa mechi ya kukumbukwa sana kwani Kobe amekuwa mchezaji maarufu sana na kati ya wachezaji wakali wa na yeye yumo.

Alishangiliwa mwanzo mwisho na mashabiki waliojitokeza kumuaga na pia watu maarufu kama Jay Z, Lamar Odom, Kendrik Lamar, Magic Johnson, Kanye West, David Beckham, Jack Nicholson, Snoop Dogg, na wengine wengi sana walikuwa ndani ya Staples Center.



Kobe amecheza na Lakers kwa misimu 20 sasa na aliingia mwaka 1996 akitokea high school akachukuliwa na Charlott Honets na baada ya muda mfupi hawakumtaka Lakers wakamchukua.

Miaka 20 amefanikiwa kushinda kombe la NBA mara 5 na kuwa MVP mara 2.



Kobe ameweja historia ndani ya Lakers na NBA kwa kuwa mchezaji bora kati ya wachezaji bora toka ligi ianzishwe.

Mke na watoto wake wawili walikuwepo kwenye game yake ya mwisho na walishangilia sana.

Aliwashukuru mashabiki wa Lakers na wachezaji wenzake baada ya game na kusema anawapenda sana na mwisho akawaaga akisema "Mamba Out!" akaweka Mic chini...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment