Wednesday 13 April 2016

NBA: KOBE BRYANT AZUA GUMZO KWENYE VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUSTAAFU KWAKE LEO


Kobe Brant au kwa jina maarufu 'The Black Mamba' amezua gumzo kubwa sana nchini Marekeni na duniani kwa ujumla kutokana na mechi yake ya mwisho leo...Kobe ni kati ya wachezaji wakali sana waliowahi kucheza NBA na aliingia kwenye ligi akiwa mdogo akitokea high school...



Kobe anaastaafu kucheza basketball leo ikiwa anaingia uwanjani na Utah Jazz na uwanja umesha furika kwani hakuna hata ticket moja imebaki...Ticket zenyewe zilikuwa bei mbaya na kuzipata kwa mbinde sana...Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu sana duniani na mashabiki wa Kobe na basketball kwa ujumla itaweka historia ya aina yake kwani watu wengi sana wataangalia jinsi anavyoagwa...


Watu kati ya 400 na 500 wa habari wamepewa nafasi ya kuingia na kutangaza siku ya leo...Kobe leo anamalizia msimu wa 20 toka aanze kucheza NBA...Usikose game ya mwisho ya mkali wa basketball Kobe Bryant leo usiku...Bofya hapa upate habari zaidi

No comments:

Post a Comment