Wednesday 6 April 2016

CHAMPIONS LEAGUE 2016: BARCELONA YATOKA NYUMA NA KUWACHAPA ATLETICO MADRID 2-1


Barcelona wameshinda mechi ambayo ilikuwa na tension toka mwanzo pamoja na vikumbo vingi...Atletico Madrid walianza kutingisha nyavu kupitia Fernando Torres lakini Torres alivyokuwa kichwa hewa akafanya ndivyo sivyo akalamba kadi ya 2 ya njano na kutolewa nje kabisa ya uwanja...Suarez ndie iliyewaokoa Barca kwa bao dakika ya 63 na dakika ya 74...Barca walichachamaa sana na kushambulia lango la Madrid mara kwa mara mithili ya nyuki wadogo...


Mabao yote ya Barca walikuwa yameenda shule kwani gonga hatari zilitembea na kuwaacha Atletico kutoa macho tu...Kinachowapa moyo Atletico Madrid ni bao la ugenini ambalo litawasaidia wakirudiana...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment