Monday 18 April 2016

LA LIGA: MESSI NA WENZAKE WACHAPWA TENA


Ubingwa wa Spain sasa uko njia panda baada ya Barcelona kula kichapo kutoka kwa Valencia 1-2...Msimamo wa ligi unawaweka Barcelona sawa na Atletico Madrid kwa points huku Real Madrid wakiwapumulia nyuma kwa point 1...Barcelona na Atletico wana points 76 na Real Madrid 75 kwahiyo kazi bado nzito kwa Barcelona...


Barcelona wamechapwa kwa mara ya 3 mfululizo na hiyo ni baada ya miaka 13 iliyopita...Valencia hivi karibuni walipokea kipigo cha mabao 7-0 kwenye copa del rey na sasa wameweza kusawazisha mambo kwa kushinda mechi yao dhidi ya Barca...


Barca sasa inabidi washinde mechi zote kama wanataka kuchukua ubingwa lakini hali ni tete...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment