Wednesday 20 April 2016

GIANNI INFANTINO: RAIS WA FIFA ANATAKA TEKNOLOJIA YA VIDEO KUTUMIKA NA MAREFA WORLD CUP 2018


Rais wa FIFAGianni Infantino, amesema anataka teknolojia ya video ianze kufanyiwa majaribia haraka sana na kama ikifanikiwa itumike katika World Cup ya 2018 huko Russia...Teknolojia ya video au kwa jina lingine 'video referees' ni kwamba marefa watakuwa wanaangalia kama walifanya makosa katika maamuzi yao au refa anaweza kuomba muamuzi wa 4 kuangalia kama makosa yalitendeka ili haki itendeke...


Kwa sasa teknolojia inayotumika ni ya golini tu...Goli likiingia muamuzi anapata ujumbe kwenye saa yake ya mkononi...Rais wa Fifa ameongea na wadau wa Russia na kuhakikishiwa kwamba pamoja na matatizo ya uchumi maandalizi ya World Cup yanaendelea vizuri...


Wadau wengi walipinga teknolijia kutumika kwenye mpira lakini dunia yetu ya sasa ni ya teknolojia kwahiyo inabidi tewnde na wakati...Bofya hapa upate habari zaidi.

No comments:

Post a Comment