Showing posts with label 2018 World Cup Russia. Show all posts
Showing posts with label 2018 World Cup Russia. Show all posts

Wednesday, 20 April 2016

GIANNI INFANTINO: RAIS WA FIFA ANATAKA TEKNOLOJIA YA VIDEO KUTUMIKA NA MAREFA WORLD CUP 2018


Rais wa FIFAGianni Infantino, amesema anataka teknolojia ya video ianze kufanyiwa majaribia haraka sana na kama ikifanikiwa itumike katika World Cup ya 2018 huko Russia...Teknolojia ya video au kwa jina lingine 'video referees' ni kwamba marefa watakuwa wanaangalia kama walifanya makosa katika maamuzi yao au refa anaweza kuomba muamuzi wa 4 kuangalia kama makosa yalitendeka ili haki itendeke...


Kwa sasa teknolojia inayotumika ni ya golini tu...Goli likiingia muamuzi anapata ujumbe kwenye saa yake ya mkononi...Rais wa Fifa ameongea na wadau wa Russia na kuhakikishiwa kwamba pamoja na matatizo ya uchumi maandalizi ya World Cup yanaendelea vizuri...


Wadau wengi walipinga teknolijia kutumika kwenye mpira lakini dunia yetu ya sasa ni ya teknolojia kwahiyo inabidi tewnde na wakati...Bofya hapa upate habari zaidi.

Thursday, 8 October 2015

2018 FIFA WORLD CUP RUSSIA: TANZANIA YAICHAPA MALAWI 2-0



Taifa Stars jana ilifurahisha mashabiki wa soka nchini kwa ushindi wa dhidi ya Flames ya Malawi 2-0...Chini ya kocha mzawa na mashuhuri Charles Boniface Mkwasa timu ya taifa iliweza kumaliza mabao yote kipindi cha kwanza kupitia star Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu...Taifa Stars wataingia jijini Blantyre tayari kwa mechi Jumapili ijayo...Bofya hapa upate habari zaidi.