Showing posts with label Divok Okoth Origi. Show all posts
Showing posts with label Divok Okoth Origi. Show all posts

Friday, 22 April 2016

LIVERPOOL: JURGEN KLOPP ASEMA MGUU WA ORIGI HAUJAVUNJIKA


Habari njema kutoka the Kop kupitia kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ni kwamba Divock Origi mguu wake haukuvika...Origi alifanyiwa foul mbaya sana na Funes Mori katika mechi ya Merseyside derby Jumatano usiku...


Klopp amesema Origi atakuwa nje kwa zaidi ya miezi 2 kwahiyo atakosa hata mashindano ya Ulaya...Bofya hapa upate habari zaidi.

Thursday, 21 April 2016

EPL: LIVERPOOL YATUPIA 4 KWENYE MECHI YA MERSEYSIDE DERBY


Liverpool FC wamefanikiwa kuwachapa wenzao Everton mechi ambayo ni derby mabao 4-0...Liverpool wanapata ushindi wa 3 mfululizo...Divock Origi ndiye aliyeanza kufungulia mabao akifuatiwa na Mamadou Sakho dakika chache badae...Kipindi cha 2 Sturridge alitupia bao na Coutinho alimalizia kwenye dakika 71...Everton walipunguzwa na kuwa 10 wakati Funes Moris alipotelewa kwa kusimama kwenye ankle ya Origi...Bofya hapa upate habari zaidi.

Friday, 15 April 2016

EUROPA LEAGUE 2016: LIVERPOOL YAIDUWAZA DORTMUND NA MASHABIKI WAKE


The Kop jana usiku paliwaka moto kwani Liverpool ilikuwa imeshajulikana inatolewa nje ya michuano ya Europa au 'Uefa ndogo' kwa msemo wa kitaa lakini la hasha...Kama umewahi kusikia timu inaitwa 'The Comeback Kings' basi jana hiko jina lilijulikana kama la Liverpool moja kwa moja...Mechi yao dhidi ya Dortmund haikuwa rahisi kabisa kwani Dortmund wamesimama na ndio walionza kufunga mabao...Liverpool mara 2 kwenye mechi hiyo walihitaji mabao matatu kufuzu...


Hali ilikuwa tete sana tena siku ambayo Liverpool walikuwa wanakumbuka miaka 27 iliyopita mashabiki 96 walipoteza maisha yao katika siku ya 'Hillsborough disaster'...Kabla mpira kuanza walitoa heshima kwa waliopoteza maisha kwa kukaa kimya kwa dakika 1...Dortmund walikuwa mbele mapema dakika ya 5 kupitia bao la Henrikh Mkhitaryan na muda mfupi badae Pierre-Emerick Aubameyang akapachika bao dakika ya 9...Mashabiki wakajua leo ndio bye bye lakini ngoma ikaendelea kuchezwa na Divock Origi aliwapa matumaini alipofunga baodakika ya 48...



Liverpool walianza kwa kushambuliwa sana na Dortmund ila badae waliweza kutulia na kucheza mpira wa maana...Reus wa Dortmund kwenye dakika ya 57 akapachika bao na kurudisha matumaini ya Liverpool nyuma....Dakika ya 60 Philippe Coutinho alifanikiwa kurudisha matumaini japi finyu lakini alibadelisha game...Dakika 10 baadda ya bao hilo Mamadou Sakho akapachika bao na sasa angalau matumaini yakarudi ingawa dakika zilikuwa zinayoyoma...


Dakika za lala salama umati wa the Kop uliruka juu kwa kushangilia sana baada ya bao la Dejan Lovren kutikisa nyavu....Kweli Liverpool imeshangaza hadi mashabiki kwa kuwa timu ambayo hata ikichapwa hurudisha mabao na kushinda...Bofya hapa upate habari zaidi.

Monday, 14 December 2015

EPL: LIVERPOOL YAOKOLEWA NA DIVOCK ORIGI DAKIKA YA 95



Liverpool ilikuwa hatiani kufungwa na West Brom baada ya bao la deflection la Mkenya Divock Origi kutingisha nyavu dakika ya 95 wakati mpira ulivyoongezwa muda wa dakika kama 10 hivi...Liverpool walianza vizuri na Jordan Henderson kupachika bao safi mapema lakini kosa la Simon Mignolet lilisababisha Craig Dawson kusawazisha...Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, alissema amefurahi na matokeo ya 2-2 kwani wanastahili hiyo point 1 waliopata...Bofya hapa upate habari zaidi.

Thursday, 3 December 2015

LEAGUE CUP: LIVERPOOL YAIRARUA SOUTHAMPTON 6-1



Liverpool yandelea kufanya vizuri chini ya kocha mpya Jugen Klopp na jana usiku walikuwa moto baada ya kuirarua Southampton 6-1 katika robo fainali ya League Cup...Daniel Sturridge alicheza jana na kujipatia mabao mawli na Mbelgiji mwenye asilia ya Kenya, Divok Okoth Origi, alipata mpira wa kupeleka nyumbani kupitia hat-trick yake...Sasa Liverpool watakutana na Stoke kwenye nusu fainali ya League Cup...


Nusu fainali itakuwa pia kati ya Everton na Manchester City...Mzunguko wa kwanza utaanza wiki ya January 4 na mzunguko wa 2 utaanza wiki ya January 25...Bofya hapa upate habari zaidi.