Manchester City wamewatoa Arsenal nafasi ya 3 na kukaa hapo baada ya kuichapa Stoke City 4-0...Mechi haikuwa na mvuto sana na Manchester City walikuwa na defense mbovu lakini pamoja na hayo waifanikiwa kuingiza mabao 4...
Bao la kwanza lilitoka kwa Fernando kupitia kichwa na la 2 lilitoka kwa Aguero dakika ya 43 kwa njia ya tuta na Iheanacho alitupia 2 kipindi cha 2...Bofya hapa upate habari zaidi.
Everton imejiweka nafasi nzuri baada ya kuwachapa Manchester City mabao 2-1...Everton ndio walioona lango la City kwenye dakika ya 45 kabla tu ya mapumziko lakini dakika ya 76 City walisawazisha kupitia Jesus Navas baada ya counter attack kali iliyosababishwa na Sergio Aguero...City walijua game itakuwa draw lakini mambo hayakuenda hivyo na ilichukua dakika 2 tu kwa Lukaku kupachika bao na kuwaweka mbele Everton...Ni bao la 12 la Lukaku kati ya mechi 12...Mechi ya jana Liverpol walishinda 0-1 dhidi ya Stoke City...Bofya hapa upate habari zaidi.
Liverpool yandelea kufanya vizuri chini ya kocha mpya Jugen Klopp na jana usiku walikuwa moto baada ya kuirarua Southampton 6-1 katika robo fainali ya League Cup...Daniel Sturridge alicheza jana na kujipatia mabao mawli na Mbelgiji mwenye asilia ya Kenya, Divok Okoth Origi, alipata mpira wa kupeleka nyumbani kupitia hat-trick yake...Sasa Liverpool watakutana na Stoke kwenye nusu fainali ya League Cup...
Nusu fainali itakuwa pia kati ya Everton na Manchester City...Mzunguko wa kwanza utaanza wiki ya January 4 na mzunguko wa 2 utaanza wiki ya January 25...Bofya hapa upate habari zaidi.
Philippe Coutinho ameipa Liverpool points 3 za mwanzo baada ya kupiga shuti kali kwa mbali...Mara ya mwisho Stoke City kukutana na Liverpool walishinda 6-1 lakini Leo wamelala kwa bao 1 la Coutinho...Bofya hapa update habari zaidi.