Max Sports brings you the latest sports news, reviews, statistics, videos, documentaries and more from across the 🌎
Showing posts with label TV rights. Show all posts
Showing posts with label TV rights. Show all posts
Wednesday, 25 May 2016
ARSENAL FC: ARSENAL NI TIMU YA KWANZA KUPATA £100 MILIONI KUTOKA PREMIER LEAGUE
Arsenal imeweka historia tena kwa kuwa timu ya kwanza katika premier league kuingiza £100 milioni kwenye Premier League msimu uliopita...Arsenal wamewapita Leicester waliomaliza wa kwanza na Manchester City...Kwa ujumla Arsenal wameingiza £100,952,257 na kati ya hizo zimo " facility fees" £21.5 milioni, zawadi ya kumaliza wa 2 kwenye ligi £23.6 milioni na zaidi ya £55 milioni za TV rights za nyumbani na nje ya nchi...Bofya hapa upate habari zaidi.
Wednesday, 6 April 2016
PANAMA PAPERS: BOSS WA FIFA GIANNI INFANTINO ATAJWA KWENYE DOCUMENTS ZA KAMPUNI ILIYOSAIDIA WATU MASHUHURI KUFICHA PESA
Gianni Infantino, Boss mpya wa FIFA, ametajwa kwenye documents ambazo zinaonyesha jinsi watu mashuhuri duniani wakiwemo maraisi na mawaziri wanavyoficha pesa kukwepa kodi...Hizo documents zinajulikana kama 'Panama Papers' na zimetoka kwenye kampuni ya binafsi ya sheria nchini Panama...
Kampuni hiyo jina lakie ni Mossack Fonseca na hizo documents ziliibiwa kupitia mitandao na sasa zimeibua mtazamo mpya kuwa kumbe watu wengi wanakwepa kodi duniani...Kwa upande wa Infantino ni kwamba hizo documents zinazungumzia watu ambao aliwahi kufanya nao mkataba zamani na hao watu wameshahusishwa na rushwa....
![]() |
| Hugo Jinkis, anahusishwa na dili la Uefa na rushwa |
Watu hao wanaitwa Hugo Jinkis na Mariano Jinkis ambao walinunua TV rights za Uefa Champions League na baada ya muda mfupi tu wakauza hizo TV rights mara 3 na kuondoka na pesa nyingi sana...Kipindi hicho mkataba huo ulipitishwa na Gianni Infantino ambae alikuwa Mkurugenzi wa Uefa...
![]() |
| Mariano Jinkis akiwa amekamatwa na polisi pamoja na mzee wake Hugo Jinkis |
Infantino amesikitika watu kumfikiria vibaya na FIFA imesema hiyo tender alishinda mwenye dau kubwa na ilikuwa halali...Bofya hapa upate habari zaidi.
Subscribe to:
Posts (Atom)




