Tuesday 11 March 2014

NBA: CLIPPERS YAFANYA VITUZ


L. A. Clippers jana iliichapa Phoenix Suns 112-105 na ushindi huu ni wa nane mfululizo...Blake Griffin alikuwa moto kwenye hiyo game na alifanikiwa kupata points 37 kabla haja 'foul out' au ametolewa nje ya game kwa kuwa na foul nyingi...Quarter ya kwanza tu alikuwa na point 22 na point guard Chris Paul alisema na yeye anashangaa na hakushtuka kwmba Griffin anapointi 22 quarter ya kwanza...Badae Griffin alitaka kuzichapa na P. J. Tucker baada ya Griffin kumwangukia Tucker kwenye paint wakigombania mpira...Mchezo ulisimama kwa muda wakati marefa wanacheki luninga kujua issue gani ilitokea....Tucker alipewa adhabu ya loose ball foul na kutolewa nje wakati Griffin aliendelea kucheza kwa muda mfupi kabla hajatoka kwa kuzidisha kiwango cha fouls...Bofya hapa ucheki zaidi...
 


No comments:

Post a Comment