Saturday 29 March 2014

F1: HAMILTON KUONGOZA MASHINDANO YA MALAYSIA GP


Dereva wa timu ya Mercedes Benz, Lewis Hamilton, ameongoza qualifying race ya mwisho na atakuwa wa kwanza mstari wa mbele kuanza mashindano hayo kesho...Lewis alimpita bingwa wa mwaka jana sekunde 0.055 kuchukua nafasi ya kwanza...Vettel na timu yake ya Red Bull wa pili na Nico Rosberg ambaye pia yuko timu ya Mercedes Benz alimpita Fernando Alonzo wa Ferrari kuchukua nafasi ya 3...Qualifying track ya leo ilikuwa inamaji sana kutokana na mvua na pia ilisababisha magari mengi kugongana na mengine kutoka nje ya track yenyewe...Lewis ni mara ya 33 sasa kuanza mbele ya grid na amefikia rekodi ya Jim Clark ambaye ni mwingereza mwenzake...Jim Clark alikuwa dereva wa timu ya Lotus na alikuwa mkali sana miaka ya 1963-1968...Alifariki kwenye ajali ya gari (Formula Two) huko Hockeinheim Ujerumani mwaka 1968...Bofya hapa upate habari zaidi...

No comments:

Post a Comment